Wazazi, vijana waeleza chanzo cha kuyumba kwa mahusiano ya ndoa

September 7, 2019 11:13 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wametoa maoni tofauti huku baadhi ya wakisema ukosefu wa elimu na uaminifu ndiyo chanzo kikubwa.
  • Teknolojia ya mawasiliano nayo yatakia kuangalia upya ili isivuruge mahusiano.
  • Vijana watakia kuwa watulivu na kutumia hekima wakati wakisaka wenza wa maisha. 

Dar es Salaam. Mahusiano ni kati ya vitu muhimu vitatu ambavyo mwanafalsafa Abraham Maslow aliainisha kama mahitaji muhimu kwa mwanadamu. 

Kama hitaji muhimu, mahusiano yana nguvu ya kuathiri utendaji wa mtu kazini, kwenye familia na hata afya yake.

Wanaotatizwa zaidi na mahusiano ni vijana kutokana na kuumizwa na watu wa karibu wakiwemo wapenzi ambao wanakusudia kuingia nao kwenye ndoa. Changamoto inayotokea zaidi ni mahusiano hayo ambayo ni rasmi na yasiyo rasmi ni kutudumu muda mrefu.   

Ni mambo gani yanayosababisha mahusiano yakose furaha na yasidumu muda mrefu? www.nukta.co.tz inakuletea majibu kutoka kwa watu mbalimbali wenye uzoefu ambayo yanaweza kukusaidia kuimarisha mahusiano yako na ya yule umpendaye. 

“Tuliwahi kuandaa harusi ya shemeji yangu na ndoa hiyo ilidumu kwa miezi mitatu ikavunjika,” anasema Verediana George mkazi wa Boko jijini Dar es Salaam ambaye mke na mama wa watoto watatu.

Verediana anasema changamoto ni kukosekana kwa uvumilivu hasa ka vijana ambao wana mtazamo mdogo kuhusu ndoa.

Ukuaji wa sekta ya teknolojia na mawasiliano ambayo imesogeza mawasiliano baina ya mtu na mtu kuwa karibu zaidi kuliko awali, nayo ni sababu nyingine ya migogoro inayotokea kwenye mahusiano.

Monica Ludaila (49), mkazi wa Jijini Dar es Salaam, amesema miaka ya zamani mahusiano yalidumu kwani wazazi waliwekeza kwenye tabia za watoto wao. Lakini kwa kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia, wazazi wengi wa sasa hawapo karibu na watoto wao.

“Ilikuwa sio rahisi kuoa mtu ambaye hajulikani kwenu. Sasa hivi kijana anaoa msichana aliemuona Facebook na Instagram miezi miwili tu wanaoana,” amesema mzazi huyo ambaye  ambaye ana miaka zaidi ya 20 kwenye ndoa.

Hata hivyo, mahusiano mengi hayajawekeza kwenye malengo na ndio sababu kubwa inayofanya mapenzi kati ya wapendanao wawili kutokudumu.


Soma zaidi:


Mahusiano ni maridhiano ya pande mbili

Khansaa Mohammed ni mtangazaji wa kipindi cha redio cha Niambie na Shujaaz, kwa mujibu wa maelezo yake, mahusiano yanatakiwa kuwa na uzito sawa kwenye pande zote mbili yaani mwanamume na mwanamke.

Amesema, siku hizi mahusiano yamekuwa  upande mmoja kwa maana ya aidha mwanamume anampenda mwanamke ambaye hampendi. Jambo hilo ni chanzo cha mafarakano hasa pale mmoja kati yao anapochoshwa na ukaribu huo.

“Mahusiano yana maana ya kuelewana na kufahamiana madhaifu na mazuri ya mtu yaani kile mvulana anataka kwa msichana kiwe kile kile msichana anataka kwa mvuluna,” amesema Mohammed.

Changamoto nyingine inayowakumba vijana ni wapenzi kukosa kuaminiana, jambo linalodhoofisha amani na kuibua malumbano yasiyo ya msingi.

Christopher Lwimbo (21) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) anasema kinachokera wengi kwenye mahusiano ni tabia ya kufuatiliana ambayo Monica amesema ni jambo zuri kufanya kabla ya kuingia kwenye ndoa na mtu yeyote. 

“Kwani hakuna kingine cha kuulizana zaidi ya uko wapi na nani?, kwanini usiniulize kazi zinaendaje? Vipi umepata kazi? Ama hata unishauri,” amesema Lwimbo.

Hata hivyo, mahusiano mengi hayajawekeza kwenye malengo na ndio sababu kubwa inayofanya mapenzi kati ya wapendanao wawili kutokudumu. Picha|Mtandao.

Ni vijana wengi ambao wanahitaji kupendwa na kuwa nafuraha wawapo kwenye mahusiano lakini huenda tafsiri ya kupendwa inatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine.

Caroline Charles (24) mhitimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam (TURDACO) amesema wavulana wengi hudhani wasichana wanataka pesa. Kuachana na pesa, muda na kujali ni kitu muhimu kwenye mahusiano.

“Binafsi ninahitaji tu kupendwa kwani ninaweza kutimiza mahitaji yangu na kutimiza ndoto zangu,” amesema Charles kuongeza kuwa mapenzi ni kujadili malengo, kushauriana na hata kupeana moyo ni jambo ambalo kila mwenye mwenza anahitaji kutimiza.

Hata hivyo, Monica amesema ni bora kila kijana afuatilie maadili na kusikiliza ushauri wa wazazi kwani vijana wa sasa wamekua wakikataa ushauri wa wazazi.

“Chukua muda kumjua mwenzi wako, fuatilia familia yao ili ujue kama anaweza heshimu ndugu zako,” amesema monica.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW