Waliopata mikopo awamu ya tatu elimu ya juu hawa hapa

October 26, 2021 2:14 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanafunzi zaidi ya 15,000 wamepata mikopo hiyo awamu ya tatu.
  • Idadi hiyo inafanya wanufaika hadi sasa kufikia 60,356.
  • Wanafunzi awamu ya tatu kutangazwa hivi karibuni.

Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya tatu yenye wanafunzi 15,261 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya Sh37.9 bilioni kwa mwaka wa masomo 2021/22.

HESLB imetoa taarifa hiyo leo Oktoba 26, 2021 ikiwa ni siku chache kabla ya vyuo vikuu kufunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo wa HESLB, Dk Veronica Nyahende amesema orodha iliyotolewa leo inafanya jumla ya wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo kufikia 60,356 ambao wamepata mkopo wenye thamani ya Sh157.3 bilioni.

Dk. Nyahende amesema, tayari HESLB imeanza kupeleka fedha za wanafunzi waliopangiwa mikopo kwa awamu zote tatu katika vyuo mbalimbali.

Wanafunzi wametakiwa kupata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mkopo maarufu kama SIPA (Student’s Individual Permanent Account) ili kujiandaa kwenda vyuoni kwa ajili ya kujisajili.


Orodha nyingine kuja baadaye

Dk Nyahende amesema orodha ya awamu ya nne itatolewa siku chache zijazo baada ya kukamilisha uchambuzi wa maombi unaoendelea na kuwataka waombaji mikopo kutembelea akaunti zao za SIPA kupata taarifa kuhusu maombi yao.

“Orodha hii ya tatu inajumuisha wanafunzi wenye sifa zikiwemo kuwa wahitaji, wameomba kwa usahihi na wamekamilisha taratibu za udahili wa chuo kimoja. Tunakamilisha uchambuzi wa maombi mengine na tutatoa orodha ya awamu ya nne siku chache zijazo,” amesema Dk Nyahende.

Serikali imetenga Sh570 bilioni kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2021/22 kwa wanafunzi 160,000 wa elimu ya juu.

Kati yao, wanafunzi 70,000 ni wanufaika wa mwaka wa kwanza na wanafunzi zaidi ya 90,000 ni wale wanaoendelea na masomo baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka. 

“Serikali imeshatupatia fedha na tumeanza kuzipeleka vyuoni … lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wanaopangiwa wanazikuta fedha vyuoni ambako watajisajili na kupokea fedha ili watimize ndoto zao,” amesema Dk Nyahende akitoa wito wa utulivu kwa waombaji wa mikopo wanaosubiri awamu inayofuata.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV