Wafahamu wanyama wanaojulikana kama ‘The Big Five’

May 29, 2026 12:56 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanaitwa ‘The Big Five’ kutokana na ugumu na hatari zao kuwawinda kwa miguu.

Dar es Salaam. Tembo, Simba, Chui, Nyati na Faru ni wanyama maarufu zaidi duniani wanaojulikana kama ‘The Big Five’. Lakinii umewahi kujiuliza ni kwanini wanyama hawa wanaitwa The Big Five? 

Je ni wakubwa kuliko wanyama wengine?

Jibu ni hapana, kwa sababu wapo wanyama wengine akiwemo Twiga ambaye ni mrefu kuliko wote, au kiboko ambaye ni mkubwa kuliko Simba, lakini hawapo kwenye orodha ya Big5

Kwanini wanaitwa hivyo ?

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) jina La Big Five halikutokana na ukubwa wa wanyama husika bali ni dhana iliyotokana na wawindaji wa zamani ambao walimaanisha wanyama hao watano ni wanyama wagumu au hatari zaidi kuwawinda kwa miguu tangu enzi za ukoloni.

Tukianza na Nyati, Tanapa wanaeleza kuwa wawindaji wengi walimuogopa sana Nyati kuliko Simba. Hii ni kutokana na kutotabirika kwake, hasira, na ghadhabu alizonazo. Mara nyingine Nyati hukufuata hata kama ukimkimbia, na hii ndio sababu mnyama huyu huitwa Mbogo.

Ikiwa wewe ni mzoefu wa kuangalia filamu za wanyama bila shaka umeshawahi kushuhudia Mbogo akimtunishia kibesi hata Simba na Simba akaufyata. Na mara nyingi Simba mmoja au wawili pekee hawawezi kumkalisha nyati.

Kwa upande wa Chui, wawindaji humwogopa kutokana na uwezo mkubwa wa uwindaji aliokuwa nao. Chui anaweza kukutazama bila ya wewe kumuona jambo linaloweza kumuweka mwindaji hatarini kushambuliwa pasina kujua saa wala sekunde. Hii ndiyo maana kumuona chui unapo talii ni ‘Big Deal’. 

Tembo ni mnyama mkubwa zaidi wa nchi kavu aliyesalia katika uso wa dunia, ana uzito mkubwa nguvu nyingi, na anauwezo wa kushambulia kwa nguvu kubwa na anapochokozwa huwa hana huruma na mtu kabisaaaaa.

Faru anaweza kuonekana mtaratibu sana lakini naweza kukimbia kwa kasi. Unapomchokoza unaweza ukajikuta pembe iliyokuwa mbele ya uso wake yote imeishia mwilini. Ukimkorofisha sahau kabisa kupanda juu ya mti kama njia ya kujiokoa kwani atakusubiri hapo chini mpaka ushuke, pona yako ni kuomba Mungu tu hasira zake zishuke aondoke.

Jambo la kuchekesha kuhusu Faru ni kwamba huwa haoni vizuri, hivyo akihisi hatari hukimbia kwanza hujihami alafu ndio hurudi kupambana.

Mfalme wa nyika, Simba sidhani kama hatari yake inahitaji kuelezewa sana, ni mnyama mwenye nguvu, ana muonekano wa kutisha na muungurumo wake tu unaweza kusikika mpaka kilomita 8 kutoka mahali alipounguruma. 

Mara nyingi Simba jike ndio huwinda zaidi, simba dume hukaa na kusubiri kula tu.

Hii ndio orodha ya the BIG FIVE, unadhani ni myama anayeweza kuongezwa kwenye orodha hii ?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

/
No matches found for this filter
29 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
29 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
29 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV

FAHAMU IDADI YA WATANZANIA WALIOOZA MENO

FAHAMU IDADI YA WATANZANIA WALIOOZA MENO

Nukta TV

"OKTOBA 29 IMTUPA FUNZO" RAIS SAMIA

"OKTOBA 29 IMTUPA FUNZO" RAIS SAMIA

Nukta TV