Wafahamu majaji 7 wa kwanza kuapa Ikulu mpya ya Dodoma

May 23, 2023 10:13 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni majaji sita wa Mahakama ya Rufaa walioteuliwa hivi karibuni.
  • Mwingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Tanzania Jaji mstaafu Rose Aggrey Teemba.
  • Rais Samia asema wameweka historia. 

Dar es Salaam. Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Ikulu mpya ya Tanzania kuzinduliwa, leo majaji sita wa Mahakama ya Rufani wamekuwa watu wa kwanza kuapa katika jengo la Ikulu hiyo iliyopo mkoani Dodoma. 

Mara tu baada ya uamuzi wa Serikali kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya Tanzania mwaka 1973 mpango ulikuwa ni kujenga Ikulu ndani ya miaka 10.

Hata hivyo, safari hiyo haikutimia ndani ya muda uliopangwa hadi Mei 20, 2023 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua Ikulu mpya na ya kisasa ya Chamwino ikiwa ni miaka 50 tangu uamuzi wa kuhamia Dodoma kufanyika. 

Mchakato huo wa ujenzi wa ikulu mpya ya Tanzania ulianza wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kuendelezwa na Marais wa awamu zote zilizopita na kukamilishwa na Rais Samia.

Historia imeandikwa tena katika Ikulu hiyo mpya ambapo majaji sita wa Mahakama ya Rufani wamekuwa watumishi wa umma wa kwanza kuapa katika jengo hilo.

Majaji hao ni Zainab Goronya Muruke, Leila Edith Mgonya, Amour Said Khamis na Dk Benhaji Shaaban Masoud. Wengine ni Jaji Gerson John Mdemu na Jaji Agnes Zephania Mgeyekwa.

Mwingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Tanzania Jaji mstaafu Rose Aggrey Teemba.

Mara baada ya kuapa, Rais Samia amewaambia kuwa wameweka historia kuapa katika Ikulu hiyo. 

“Karibuni Ikulu mpya na hongereni kwa kuweka historia. Ndio wa mwanza kuapa hapa, nadhani kila mtu akipata picha yake atasema nikiwa jaji wa kwanza wa mahakama kuapa Ikulu mpya muweke wajukuu waje waione,” amesema Rais Samia. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV