Vunja mbavu zako na filamu ya “Hubie Halloween”

October 9, 2020 7:21 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayofundisha kutokufanya maamuzi kwa kumdharau mtu kwa muonekano wake.
  • Inamhusu Hubie ambaye analazimika kufunga safari ya kuokoa mtaa wake.
  • Baba huyo ambaye haaminiki kwa lolote na wenzake, analazimika kufanya upelelezi wa kesi ya mauaji iliyotokea mtaani hapo.

Dar es Salaam. Umejiandaaje kuvunjwa mbavu zako kwa burudani? Mchekeshaji wa Marekani, Adam Sandler anaingia ulingoni na filamu ya  Hubie Haloween kwa ajili ya kurudisha kicheko chako.

Kama ilivyo kawaida kwa nchi za magharibi, Oktoba 31 kila mwaka watu huadhimisha sikukuu ya Haloween ambapo watu huvalia mavazi mbalimbali yakiwemo ya kutisha ikiwa ni maadhimisho yanayofanyika kufukuza na kujikinga na mizimu.

Hali ndivyo ilivyo kwenye filamu ya  Hubie Haloween ambapo Hubie Dubois (Adam Sandler) amekuwa ni mtu anayeandamwa na kila mtu anayetaka kumwekea mtego mtu.

Wakati sikukuu ikikaribia, Dubois ananusa harufu ya mauaji na hivyo kuanza kufuatilia mauaji hayo.

Dubois huyo huyo ambaye amegeuka kuwa kituko mbele ya jamii yake, anawezaje kuaminika kuwa anaongelea jambo la kweli?


Soma Zaidi:


Baada ya kuona kuwa yeye ndiye msaada pekee, anaamua kuvaa viatu na kuanza upelelezi wake.

Atafanikiwa? Ataaminika? Je, upelelezi wake utavumbua ukweli?

Usikose filamu hii iliyoandaliwa chini ya Netflix huku ikiwa bado mpya mtandaoni humo ikiambatana na nyota wachekeshaji kutoka kwenye filamu maarufu kama Grown Ups, Stranger Things, Modern Family na Zoo Keeper.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV