Vipaumbele 10 vya bajeti ya wizara ya kilimo 2020-21, fedha zikipungua

May 12, 2020 4:49 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Vipaumbele hivyo vinalenga kuimarisha usalama wa chakula na malighafi za viwanda.
  • Bajeti ya wizara hiyo imeshuka kidogo hadi Sh229.8 bilioni mwaka 2020/21 kutoka 253.8 mwaka 2019/2020. 

Dar es Salaam. Bunge la Tanzania limeidhinisha Sh229.8 bilioni kwa ajili ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 ambayo inakusudia kutekeleza vipaumbele 10 ikiwemo kuzalisha mbegu bora kwa ajili ya wakulima wa Tanzania.

Bajeti hiyo ambayo itaanza kutekelezwa Julai 1 mwaka huu imeshuka kidogo kwa Sh24.1 bilioni kutoka Sh253.8 bilioni ya mwaka 2019/2020. 

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga katika hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka ujao wa 2020/21 amesema vipaumbele hivyo vitasaidia kuimarisha sekta ya kilimo nchini ili ichangie katika uchumi wa viwanda.

“Mpango wa bajeti umeweka msisitizo kwenye kilimo kitakachohakikisha usalama wa chakula ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula na upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda,” amesema Hasunga. 

Hasunga amesema amezitaja vipaumbele hivyo kuwa ni wizara kuendelea na utekelezaji wa progamu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) ambayo inalenga kuimarisha vyuo na vituo vya mafunzo na utafiti vya kilimo, udhibiti wa visumbufu vya mimea, huduma za ugani, usajili wa wakulima na bima ya mazao. 


Soma zaidi: 


Waziri huyo amesema kipaumbele kingine ni kuboresha mifumo ya kitaasisi, bodi na sheria za kilimo kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa

maendeleo ya mazao ya kilimo na kuunganisha wakulima wadogo na mashamba makubwa ili kuendeleza kilimo cha kibiashara.

“Tutawapatia ujuzi na maarifa ya kilimo chenye tija, kurahisisha upatikanaji wa huduma za pembejeo na masoko, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji, maghala, masoko na miundombinu ya kuhifadhi mazao ya kilimo,” amesema Hasunga. 

Watendaji wa wizara hiyo pia watakuwa na kibarua cha kuimarisha uzalishaji wa mbegu bora za mazao na upatikanaji wa pembejeo nyingine za kilimo na kuzisambaza kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa mazao.

Maeneo mengine yatakayopewa kipaumbele, Hasunga amesema ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa maendeleo ya ushirika pamoja na kuweka mifumo itakayoongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wanaushirika na wadau wengine wa sekta ya kilimo.

“Tutaongeza matumizi ya teknolojia bora katika uzalishaji wa mazao na tija, kuimarisha vituo vya utafiti, vyuo vya mafunzo na vituo vya mafunzo kwa wakulima kwa kujenga miundombinu wezeshi na kuboresha maarifa na ujuzi kwa watafiti, wakufunzi na wazalishaji kwa lengo kukuza kilimo,” amesema waziri huyo. 

Ili kuhakikisha ardhi inatumika vizuri, wizara ya kilimo katika mwaka 2020/21 itaimarisha huduma za upimaji wa matabaka na ubora wa udongo ili kuendana na mahitaji ya mazao ya kilimo kimaeneo. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akikagua miche ya mkonge hivi karibu alipotembea kituo cha TARI mkoani Tanga. Picha|Wizara ya Kilimo.

Mbunge wa Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage amesema katika vipaumbele vya wizara hiyo amependekeza Serikali kuhakikisha inawekeza katika kuweka miradi ya kimkakati kuzalisha chakula kingi hasa mazao ya nafaka ili kuondoa uhaba wa chakula nchini.  

“Tukiyazalisha (mazao)tuwe na vihenge vikubwa vyenye uwezo wa kuhifadhi nafaka nyingi ambavyo vinaweza kuwezesha nchi hii kuwa na chakula cha kutosha kwa miaka mitatu au minne,” amesema Mwijage ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Hata wakati wizara hiyo ikiainisha vipaumbele hivyo, Waziri Hasunga hajaweka wazi ni kiasi gani cha pesa wizara yake ilichopatiwa mpaka sasa katika bajeti ya mwaka 2019/2020.

 Kilimo ndiyo shughuli kuu inayotegemewa na sehemu kubwa ya Watanzania baada ya Ripoti ya utafiti wa masuala ya kifedha ya Finscope ya mwaka 2017 kubainisha kuwa asilimia 41 ya Watanzania wanategemea shughuli za kilimo kama chanzo cha mapato kuendesha maisha.

Pamoja na kuwa ndiyo uti wa mgongo, kilimo kimekuwa kikikua kwa kasi ya kobe chini ya wastani wa ukuaji wa uchumi wa Taifa wa wastani wa asilimia saba. 

Kwa mujibu wa kitabu cha hali ya uchumi kwa mwaka 2018, kilimo kilikuwa kwa asilimia 5.3 mwaka 2018 nyuma ya viwanda jambo linalofanya wengi wasiguswe vema na ukuaji wake.  

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV