Vijiji zaidi ya 7,000 vyapatiwa umeme Tanzania

June 13, 2019 9:09 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Waziri Mpango amesema Vijiji 7,127 vimeunganishwa na umeme.
  • Njia za kusambaza umeme za msongo wa kV 33 zenye urefu wa kilomita 18,227 zimejengwa.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameliambia Bunge leo jijini Dodoma kuwa uzalishaji wa umeme umeongezaka nchini kutoka GWh 7,092.13 mwaka 2015/2016 hadi GWh 7,374 mwaka 2018/2019 huku vijiji zaidi ya 7,000 vikiwa vimeunganishwa na nishati hiyo.

Dk Mpango amesema ongezeko hilo la uzalishaji wa nishati hiyo limechangia kuongezeka kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika.

“Kuongezeka kwa kasi ya usambazaji umeme vijijini hadi kufikia Mei 2019 jumla ya vijiji elfu 7,127   vimeunganishwa umeme ambapo jumla ya taasisi za elimu 3,165, maeneo ya biashara 3,451 pampu za maji 210 taasisi za afya 1,211 na nyumba za ibada 984 zimeunganishwa umeme,” amesema Waziri Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya Hali ya Uchumi mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2019/2020.

Hii ni sawa na ongezeko la vijiji 5,109 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ambalo ni ongezeko la asilimia 253 ya vijiji vilivyokuwa na umeme kufikia mwaka 2015. 


Zinazohusiana:


Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya mwaka 2019/2020, ifikapo mwezi Juni, 2020 vijiji zaidi ya10,278 kati ya 12,268 vya Tanzania Bara vitaunganishwa umeme sawa na asilimia 84 ya vijiji vyote.

Dk Mpango amesema mafanikio mengine ni kufikishwa umeme katika vijiji vya wilaya na Halmashauri 15 pamoja na ujenzi wa njia za kusambaza umeme za msongo wa kV 33 zenye urefu wa kilomita 18,227 sambamba na ujenzi wa vituo vidogo vya kupoza na kusambaza umeme 4,100. 

Pia ujenzi wa njia ndogo ya usambazaji umeme zenye urefu wa kilomita 30,797.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV