Epuka kupigwa: WHO haitoi fedha za Corona

January 2, 2021 10:24 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Shirika hilo la afya limezushiwa kuwa limetangaza kutoa fedha za kupambana na Corona kwa kutumia tovuti feki.
  • Hata hivyo, tovuti rasmi ya WHO haijatoa tangazo hilo. 
  • Wananchi wanatakiwa kuwa makini na utapeli unaofanywa kupitia janga la Corona. 

Dar es Salaam. Utapeli wa mtandaoni unaofanywa kwa mgongo wa janga la Corona unazidi kushika kasi duniani na kwa mara nyingine tena  Shirika la Afya Duniani (WHO) limezushiwa kuwa limetangaza kutoa msaada wa fedha kwa ajili ya mapambano ya virusi vya COVID-19.

Taarifa iliyotolewa katika tovuti isiyo kuwa ya WHO, inasema Shirika hilo linatoa msaada wa fedha kiasi cha Euro 500 (Sh1.5 milioni) kwa ajili ya watu, kampuni au taasisi zinazopambana na ugonjwa wa Corona.

Hata hivyo, habari hiyo haina ukweli wowote kwa sababu shirika hilo halijatangaza msaada huo wa fedha. 

Taarifa hiyo iliyopo kwa mfumo wa kiunganishi (Link) imeandikwa kwa lugha ya kiingereza kuwa “You have been selected to benefit from the support provided by the World Health Organization for 500 Euros” inayomaanisha “Umechaguliwa kunufaika na msaada wa Euro 500 uliotolewa na WHO”

Tovuti hiyo inamtaka mtu kujaza taarifa zake muhimu ikiwemo kama ni mfanyakazi, hali ya ndoa (ameolewa au kuoa), umri, kisha kutakiwa kuwashirikisha marafiki kuingia kwenye tovuti hio ili na wao wapate msaada huo.

Kwanini tovuti hiyo ni feki?

Tovuti iliyotumika kutoa taarifa hiyo haina uhusiano kabisa na ile tovuti rasmi ya WHO. Tovuti hiyo ina kikoa cha https://vip-l97.work/dn/?th=#1609580327292, wakati tovuti rasmi ya WHO ambayo ndiyo ina taarifa zote za Corona ni https://www.who.int/.

Eneo nyingine linalothibitisha kuwa tovuti hiyo siyo ya kweli ni kuwataka watu kutuma taarifa zao binafsi, jambo ambalo ni kinyume na sheria za usiri za kimataifa. 

Pia inawashurutisha watu waisambaze kwa watu wengi. Suala kusambaza taarifa ni hiari na halipaswi kuwa la lazima. 

Kwa mantiki hiyo, tovuti na taarifa hiyo haijatolewa na WHO kwa sababu timu ya #NuktaFakti imetembelea tovuti na mitandao ya kijamii ya shirika hilo leo Januari 2, 2020 na haijafanikiwa kupata taarifa ya namna hiyo.  


Zinazohusiana:


Hii ni mara ya pili Shirika hilo kuzushiwa taarifa ya uzushi baada ya Julai 9, 2020 kuzushiwa kwamba imetangaza nafasi za kazi ili kupambana na Corona.

Kama umekutana na taarifa hiyo, usiwe mwepesi wa kusambaza kwa watu wengine kabla ya kujiridhisha kama ni kweli ili kupunguza madhara ya habari za uzushi kwenye jamii. 

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks