Uzalishaji dhahabu waongezeka, mauzo nje ya nchi yakishuka

June 29, 2022 2:45 pm · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Uzalishaji wa dhahabu kwa mwaka 2021 ulikuwa kilogramu 59,638 kutoka kilogramu 55,805 mwaka 2020.
  • Mauzo nje ya nchi mwaka jana yalipungua kwa asilimia 13.9.
  • Athari za Uviko-19 na kupungua kwa uzalishaji katika baadhi ya migodi kwachangia.

Dar es salaam. Licha ya uzalishaji wa dhahabu kuongezeka kwa asilimia 6.9 mwaka mmoja uliopita, kiasi cha madini hayo kilichouzwa nje ya nchi yameshuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo janga la Uviko-19.

Kwa mujibu wa Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 kilichotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) hivi karibuni, uzalishaji wa dhahabu kwa mwaka 2021 ulikuwa kilogramu 59,638 ambapo umeongezeka kutoka kilogramu 55,805 zilizozalishwa mwaka 2020.

Hilo ni ongezeko la kilogramu 3,833 au asilimia 6.8 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. 

NBS imeeleza kuongezeka kwa uzalishaji wa madini hayo kumechangiwa na kuongezeka kwa uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu iliopo mkoani Shinyanga ambapo ulifikia kilogramu 4,864 mwaka 2021 kutoka kilogramu 1,553 mwaka juzi.

“Kuimarika kwa usimamizi wa wachimbaji wadogo wa dhahabu kupitia masoko na vituo vya ununuzi,” kitabu hicho kimeeleza.

Madini ya dhababu hutumika katika usafishaji wa madini mengine kama Almasi na Tanzanite, kutengeneza mapambo na vito lakini pia hutumika kuonyesha thamani ya fedha kwa nchi mbalimbali duniani.


Zinazohusiana:


Uuzaji dhahabu nje ya nchi, umeshuka

Kati ya kiasi cha dhahabu kilichozalishwa mwaka jana, ni kilogramu 42,902 za dhahabu zilizopata vibali vya kusafirishwa nje ya nchi ikilinganishwa na kilogramu 49,812 zilizopata vibali mwaka 2020, sawa na upungufu wa asilimia 13.9.

NBS katika kitabu hicho kinachotoka kila mwaka imesema kuwa thamani ya dhahabu iliyopata vibali vya kuuzwa nje ya nchi ilipungua kwa asilimia 0.5 na kufikia Dola za Marekani 2,831.8 milioni sawa na pesa za kitanzania Sh6.55 bilioni ikilinganishwa na Dola za Marekani  2,844.9 milioni mwaka 2020 sawa na Sh6.58 bilioni.

Kushuka kwa uuzaji wa dhahabu nje ya nchi, kumetokana na kupungua kwa biashara ya madini ya dhahabu katika soko la dunia kulikosababishwa na athari za Uviko-19. 

Sababu nyingine ni kupungua kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu baada ya kufungwa kwa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi pamoja mgodi mmoja katika mgodi wa dhahabu wa Geita.

Mikakati ya Serikali kuongeza uzalishaji 

Waziri wa Madini Dotto Biteko katika hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2022/23  alisema miongoni mwa vipaumbele vya wizara yake ni kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli na kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa.

“Tutawaendeleza wachimbaji wadogo na kuwawezesha wananchi kushiriki katika uchumi wa madini, kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini, kuhamasisha biashara na uwekezaji katika sekta ya madini pamoja na kusimamia mfumo wa ukaguzi wa shughuli za migodi,” alisema Waziri Biteko.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV