Utupaji sigara hovyo unavyoathiri binadamu, viumbe wa baharini

February 7, 2022 12:03 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kampeni maalum yazinduliwa kukabiliana na vitendo vya utupaji sigara hovyo.

Dar es Salaam. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira UNEP limezindua kampeni ya kujenga uelewa na kuchukua hatua za kutunza mazingira na afya za wananchi kutokana na vipande vidogo vidogo vya plastiki katika machujio ya sigara.

UNEP inashirikiana na Sekretarieti ya Mkataba wa Mfumo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani juu ya Udhibiti wa Tumbaku (WHO FCTC) katika kampeni hiyo itakayofanyika mtandaoni na inayohusisha kutumia watu maarufu na vijana wachechemuzi wa masuala ya mazingira mitandaoni na mabalozi wa hiyari.

Ushirikiano huo unawezeshwa kupitia kampeni ya UNEP ya “Bahari Safi”, muungano wa kimataifa unaojumuisha nchi 63 zinazojitolea kukomesha uchafuzi wa plastiki baharini.

Mkuu wa Uhamasishaji wa Umma wa UNEP Atif Butt amesema, “Sekretarieti ya WHO FCTC ina utaalamu wa kiufundi wa athari za bidhaa za tumbaku siyo tu kwa afya ya binadamu bali pia kwa mazingira, kwa kujiunga nasi  katika uanzishaji wa Bahari Safi bila vipande vya plastiki, tunalenga kuangazia jinsi afya yetu inavyohusishwa na ile ya sayari yetu.”

Kila mwaka, tasnia ya tumbaku huzalisha sigara trilioni 6 zinazotumiwa na wavutaji sigara bilioni 1 duniani kote. 

Sigara hizi zina vichujio vinavyojumuisha hasa plastiki ndogo zinazojulikana kama nyuzi za acetate za selulosi. Sigara zinayotupwa hovyo vitako yake ( Vichungi)  huvunjika kutokana na sababu mbalimbali kama mwanga wa jua na unyevunyevu na hapo ndiyo hutoa plastiki ndogo pamoja na kemikali nyingine nyingi, hivyo kuathiri afya na huduma za mifumo ikolojia.

Mkuu wa Sekretarieti ya WHO FCTC, Adriana Blanco Marquizo amesema, “Nawaomba nyote kujiunga na kampeni hii. Hebu sote tufanye sehemu yetu kuhakikisha bahari yetu pamoja na wakazi wake wote  wanalindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.”

Ushirikiano huu unaashiria hatua muhimu ya kwanza kuelekea kupata  suluhisho la athari za kiafya na kimazingira za plastiki ndogo kwenye vichungi vya sigara.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Nukta TV

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Nukta TV

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Nukta TV