Unatumia saa ngapi kufanya kazi kwa wiki?

January 5, 2023 11:47 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Wafanyakazi wanaolipwa na waliojiajiri wenyewe (wenye wafanyakazi na wasio na wafanyakazi) wanatumia muda mwingi kazini ikilinganishwa na makundi mengine.

Dar es Salaam. Licha ya muda wa kufanya kazi kwa watu waliopo kwenye ajira kupungua Tanzania, wafanyakazi wanaolipwa na waliojiajiri wanafanya kazi muda mwingi kuliko makundi mengine.

Kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa Uwezo wa Kufanya Kazi Tanzania (ILFS) ya mwaka 2020/21 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (OCGS), muda wa kawaida wa kazi umepungua kidogo kutoka wastani wa saa 54 kwa wiki mwaka 2014 hadi saa 53 mwaka 2020/21.

Kupungua kwa muda wa kawaida wa kazi kati ya mwaka 2014 na 2020/21 kumeonekana zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Hali hii inachangiwa na wanawake kutumia muda mwingi katika shughuli za kijamii. 

Hata hivyo, masaa ya kufanya kazi yanaendana na viwango vya kimataifa vinavyotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) vya kufanya kazi kati ya saa 48 na 56 kwa wiki.

Aidha, matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa wafanyakazi wanaolipwa na waliojiajiri wenyewe (wenye wafanyakazi na wasio na wafanyakazi) wanatumia muda mwingi kazini ikilinganishwa na makundi mengine.

Saa za kazi ni kipimo cha wastani wa muda ambao watu hutumia kwenye shughuli za uzalishaji wa bidhaa na huduma. Uchambuzi wa muda wa kazi umefanyika kwa kuangalia Saa za Kazi za Kawaida (Usual Hours of Work) na Saa za Kazi za Sasa (Current Hours of Work).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV