Unafikiri kila mapenzi ni mahaba? Filamu ya “The Half of It” ni tofauti

May 8, 2020 12:29 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayoelezea kisa cha mahaba ya binti Elle Chu ambaye asili yake inamtenga na wengine.
  • Kupitia kazi ya kuandika barua za mapenzi, anajikuta akikutana na mtu anayeelewa hisia zake.
  • Hata hivyo hisia zote zinageuka machozi kwani siyo kila pendo ni la kupenda.

Dar es Salaam. Ni mara ngapi umesema wewe mapenzi hayajaumbwa kwa ajili yako? Huenda hauwezi hata kuhesabu.

Kama wewe upo kwenye hali hiyo, huna budi kufuatilia kisa hiki cha Ellie Chu Ambaye anajiweka mbali na ulimwengu wa mahaba huku ndiyo kwanza akiwa na miaka 17 tu. 

Kinapatikana katika filamu ya “The Half of It” iliyojaa visa vingi vya kusisimua. 

Chu ambaye hajafanikiwa kuzoeana na mtu yeyote chuoni, anajikuta akijitenga kwa sababu yupo tofauti na wenzake. Chu ni msichana pekee mwenye asili ya China kati ya wanafunzi wa Marekani waliopo chuoni hapo.

Hata hivyo, mbali na ukimya wake, Chu ni mwandishi mzuri hivyo anafanya kazi ya kuwaandikia watu insha zao za kitaaluma. Kwake kupata Sh138,852 kwa kazi hiyo ni kugusa tu. 

“Sijawahi kufikiria kama ninahitaji mtu mwingine kwenye maisha yangu,” ni maneno ya Chu.

Huenda alisema maneno hayo bila kufikiri kwani ghafla mambo yanabadilika pale anapoanza kumuandikia mtu  barua za mahaba.

Ndiyo Chu aligeuka kuwa msaada kwa barobaro mmoja ambaye mdomo wake ulikuwa mzito kuwasiliana na binti ambaye moyo wake umemdondokea.


Zinazohusiana


Andiko hadi andiko na ndipo asali inapomwagikia kwenye chai.

Hata baada ya Chu kufikiri amepata mtu anayemuelewa, kumbe ndiyo amejitumbikiza kwenye shimo la usaliti.

Nani amemsaliti nani? Ni kazi kwako kufahamu kisa hiki katika filamu ya  The Half of It ambacho bado kinafuka moshi kwenye mtandao wa Neftlix.

Wiki ijayo kuna nini? Usicheze mbali na ukurasa huu.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

Nukta TV

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Nukta TV