Umoja wa Ulaya kuanza kutumia chanja aina moja za simu

June 8, 2022 7:40 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Lengo ni kutunza mazingira na kurahisisha upatikanaji wake.
  • Zitaanza kutumiaka mwaka 2024 katika nchi zote za umoja huo. 
  • Sheria itaanza kutumika rasmi 2024.

Dar es salaam. Dar es Salaam. Umoja wa Ulaya (EU) umepitisha azimio la kutumia chaja zinazofahamika kama ‘type C’ kwenye simu zote pamoja na vifaa vya umeme vya kuchajiwa vitakavyouzwa ndani ya umoja huo ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

EU imesema mchaja hizo zitasaidia kupunguza uchafu wa taka za kielektroniki pamoja na kurahisisha maisha ya watumiaji.

Bunge la EU limeeleza kuwa chini ya sheria mpya,  watumiaji wa chaja aina C hawatalazimika kuwa na chaja tofauti tofauti za vifaa vya umeme wala kununua chaja  pale wanaponunua vifaa vipya kwani chaja moja inaweza kutumika kwenye vifaa tofauti. 

Taarifa ya bunge hilo iliyotolewa Juni 7, 2022 imebainisha kuwa utekelezaji wa sheria hiyo unaotarajiwa kuanza mwaka 2024 na utasaidia kuokoa kiasi cha Euro milioni 250 (Sh6.4 trilioni) kutokana na manunuzi yasiyo ya lazima ya chaja.


Soma zaidi: 


Makampuni ya utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki kama vile simu za mkononi, kamera, vishikwambi na spika za masikioni wataanza kutekeleza sheria hiyo mwaka 2024 huku wakijiandaa na mabadiliko ya chaji za kompyuta mpakato katika miezi 40 ijayo.


Hali itakuaje kwa watumiaji wa iPhone?

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya  inaeleza kuwa mwaka 2020 takribani chaji milioni 450 ziliuzwa kaika umoja huo ambapo karibu theluthi mbili ya watumiaji walipatwa na changamoto za kimatumizi

Kamisheni hiyo inaeleza kuwa  katika muongo uliopita umefanikiwa kupunguza idadi ya chaja za simu kutoka 30 mpaka tatu, ingawa changamoto kubwa ipo kwa watumiaji wa bidhaa za Iphone ambazo ni karibu na asilimia 20 za soko la bidhaa za kielektroniki barani Ulaya. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV