Ujumbe wa Rais Samia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum Tanzania

March 7, 2022 11:43 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Wanafunzi wa Shule ya uhuru Mchanganyiko na Uhuru Msingi zilizopo eneo la Gerezani Ilala Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Machi, 2022. Picha| Ikulu.


  • Awataka kusoma kwa bidii na kupigania kesho yao.
  • Asema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ili wasome katika mazingira rafiki.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema licha ya changamoto za kimaumbile na miundombinu zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalum wanatakiwa kusoma kwa bidii ili kuzifikia ndoto zao wakati Serikali ikiwaboreshea mazingira ya kusomea.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza leo Machi 7, 2022 alipotembelea Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam amesema wanafuzi wenye mahitaji maalum wana uwezo mkubwa kama walivyo wanafunzi wa kawaida, hivyo wazipiganie ndoto zao kikamilifu.

“Mna uwezo wa kufanya mambo makubwa kwa ajili yenu…,” amesema Rais Samia na kuongeza kuwa kila mtu ana kipaji chake ambacho mtu amempa bila kujali mapungufu ya kimaumbile.

“Nawaomba msome kwa bidii, mpate elimu baadaye kila mmoja achugue nini anaweza kufanya, Serikali yenu ipo itakuja kuwaunga mkono.”

                   

Amesema Serikali inaendelea kuboresha elimu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwemo kuwajengea miundombinu rafiki, vifaa vya kusomea na kuwapatia walimu wenye ujuzi wa kufundisha.

Aidha, amesema Serikali imeandaa miongozo ya kurahisisha utoaji wa elimu maalum na jumuishi nchini. Miongozi hiyo ni pamoja na mongozo wa majengo ya Serikali yanayozingatia mahitaji ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wa mwaka 2020 na mwongozo wa lishe shuleni wa mwaka 2021.

“Pamoja na kujenga shule na madarasa ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na jumuishi, Serikali imeshatumia zaidi ya Sh5.9 bilioni kununua vifaa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika elimu msingi, sekondari na vyuo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV