Uhaba, mgao wa maji ulivyoziweka rehani afya za watu Dar-2

December 10, 2022 7:59 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wataalam wa afya washauri watu waendelee kuchukua tahadhari.
  • Watu washauriwa kuchemsha maji, kutibu maji kwa dawa.

Dar es Salaam. Baada ya kuangazia changamoto za kiafya walizopitia baadhi ya watu kutokana na mgao wa maji katika jiji la Dar es Salaam, leo tunaendelea kuangazia tahadhari ambazo zinapaswa kuchukulia hata baada ya mgao huo kuisha.

Watalaam wa afya wanaeleza kuwa huenda madhara ya kiafya waliyopata watu yangepungua kama wangejenga utamaduni wa kuzingatia kanuni za afya ikiwemo kuepuka kunywa maji yasiyochemshwa. 

Daktari Joshua Sultani kutoka hospitali ya Ahmadiyya ya mkoani Morogoro  anasema kuchemsha maji ya kunywa ni moja kati ya njia ya kujilinda na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuhara yanayochangiwa na kutumia maji yenye vimelea vya wadudu. 

“Mbinu ya kwanza ni kupunguza maambukizi kwenye maji kwa kuyachemshaa ikiwa ni ya kunywa,” anasema Dk Sultan na kusisitiza kuwa kuwa kuongeza dawa za kuua vijidudu (disinfectant) kama vile kwenye maji ya kuoga na kunywa kunamuweka mtumiaji salama dhidi ya magonjwa.

Moja kati ya madhara waliyopata wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakati wamgao wa maji ni kupata vipele na maambukizi ya bakteria kwenye ngozi. Picha|Lucy Samson.

Chukua tahadhari

Hata wakati mgao kupungua na maji ya bomba yanayosambazwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Dawasa) kuanza kutumika kama awali, bado watu wanasisitizwa kuendelea kuchukua tahadhari ya namna wanavyotumia maji hayo katika shughuli mbalimbali ikiwemo nyumbani.

“Kwa ufupi maji  yanatoka kwenye bomba kwa sasa si salama, kwa sababu lile bomba linakuwa limekaa muda mrefu bila kutoa maji kwa hiyo linakuwa limebeba kutu, bakteria na vijidudu vingine,” anasema Dk Emmanuel Shayo kutoka zahanati ya Arafa iliyopo Bunju A  jijini Dar es Salaam.

Daktari huyo anawashauri wakazi wa jiji hilo kutojisahau na kuhakikisha wanatibu maji ili kuepuka magonjwa. 

“Hata kama Dawasa wana utaratibu wa kuua vijidudu hatarishi kwenye maji ni vyema kama tukiongeza jitihada kwa kufanya wenyewe ili kulinda afya zetu,” anasisitiza Dk Shayo.

Dk Shayo anasema tahadhari hizo zikizingatiwa zitasaidia kupunguza watu wanaokwenda kutibiwa hospitali ili watu waendelea kufanya shughuli za maendeleo wakiwa na afya bora. 

Sera ya Maji ya mwaka 2002 inaeleza kuwa upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya za wananchi. 

Utumiaji wa maji ambayo siyo salama na uhaba wa maji huchangia katika kusababisha milipuko na kuenea kwa magonjwa kama kuhara na kipindupindu. 

Aidha, wingi wa maji yanayofaa kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi una kikomo, na maji hayo pia yanaweza kuathirika kirahisi. Maji yanayofaa yanaendelea kupungua siku hadi siku kutokana na kuongezeka kwa mahitaji, inaeleza sera hiyo.


Zinazohusiana;


Juhudi za kimataifa kutibu maji

Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na serikali duniani kama mlezi wa afya za watu duniani linaongoza juhudi za kimataifa za kuzuia maambukizi ya magonjwa yatokanayo na maji, na kushauri serikali juu ya maendeleo ya malengo na kanuni za afya.

“Tangu mwaka 2014 WHO imekuwa ikifanya majaribio ya bidhaa za kutibu maji ya kaya kupitia mpango wa kimataifa wa WHO wa kutathmini teknolojia za matibabu ya maji ya kaya,” linasema shirika hilo. 

WHO inafanya kazi kwa karibu na UNICEF katika maeneo kadhaa yanayohusu maji na afya. Kwa mfano, mpango wa utekelezaji wa kimataifa wa kukomesha vifo vya watoto vinavyoweza kuzuilika kutokana na nimonia na kuhara ifikapo mwaka 2025 (GAPPD).

Sambamba na mradi huo shirika hilo linafanyia kazi malengo kadhaa ya kinga na matibabu, ikiwa ni pamoja na kufikia upatikanaji wa maji ya kunywa kwa wote katika vituo vya huduma za afya na majumbani ifikapo 2030.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV