Uchaguzi Serikali za Mitaa kufanyika Novemba 27, 2024

August 15, 2024 1:23 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Kura zitaanza kupigwa saa mbili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni.
  • Serikali yaahidi uchaguzi huru na haki.

Dar es Salaam. Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa amesema uchaguzi wa Serikali wa Mitaa utafanyika Novemba 27, 2024 ambapo kura zitaanza kupigwa majira ya saa mbili asubuhi na kumalizika saa 10 kamili jioni.

Mchengerwa amewaambia wananchi leo Agosti 15, 2024 kuwa kampeni za uchaguzi huo zitafanyika siku saba kabla ya uchaguzi yaani kuanzia Novemba 20 – 26, 2024 ambapo vyama vyote vya siasa vitatakiwa kuwasilisha ratiba ya kampeni zao kwa msimamizi wa uchaguzi siku saba kabla ya kampeni.

“Ninautangazia umma wa Watanzania, nawatangazia viongozi vyama, navitangazia vyama mbalimbali vya siasa kote nchini vyenye usajili wa kudumu kuwa tarehe 27, Novemba 2024 itakuwa siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara. Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni.” amesema Mchengerwa.

Kwa mujibu wa Mchengerwa katika uchaguzi huo viongozi wanaotarajiwa kuchaguliwa ni pamoja na mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa kamati ya halmashauri ya kijiji pamoja na wenyeviti wa vitongoji.

Mchengerwa ameongeza kuwa uchaguzi huo utafuata sheria na kanuni za uchaguzi zinazozingatia haki, uwazi, na usawa kwa watu wote sambamba na kutoa elimu ya upigaji kura kwa wananchi kuanzia kesho Agosti 16, ambapo amezitaka taasisi zitazotaka kushiriki zoezi hilo kuzingatia muongozo uliotolewa na Tamisemi.

Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi, Adolf Ndunguru ameuhakikishia umma kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki kwa kuwashirikisha wadau wote wa siasa nchini.

“Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imefanya kazi yote ya maandalizi ya uchaguzi ikiwemo kuandaa nyaraka zinazohitajika kwa kushirikisha wadau kwa asilimia 100 hadi tulipofikia,” amesema Ndunguru.

Kwa muda mrefu wadau wa siasa wamekuwa wakiiasa Serikali kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki ya uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa 2024 kwa kuzingatia haki na sheria ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV