Tamisemi yaongeza muda wa rufaa wagombea uchaguzi Serikali za Mitaa 2024
- Muda waongezwa kwa siku mbili ambao utakoma Novemba 15, 2024.
- Ni mara baada ya CCM kuiomba Tamisemi ipuuzie makosa madogo.
Arusha. Huenda wagombea walioenguliwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 wakapata ahueni mara baada ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusogeza mbele muda wa kupokea na kutoa majibu ya rufaa zao.
Uamuzi huo wa Tamisemi umekuja saa chache tu mara baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu waka Emmanuel Nchimbi kuiomba wizara hiyo inayosimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kupuuzia makosa madogo ya wagombea ili kutoa nafasi kwa wagombea wengi zaidi kuwania nafasi zao jambo litakalosaidia kukuza demokrasia.
Kwa mujibu wa Tamisemi uamuzi huo umetokana na maoni mbalimbali waliyopokea kutoka kwa wadau wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa vikiwemo vyama vya siasa kuhusu mchakato wa uteuzi na ushughulikiaji wa pingamizi za wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.
Tamisemi imesema miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa ni pamoja na na muda wa kuwasilisha na kutoa maamuzi ya rufaa za wagombea ambao hawakuteuliwa ambapo kwa mujibu wa ratiba ya awali ulikuwa unatamatika leo Novemba 13, 2024.
Kupitia taarifa aliyoitoa kwa wanahabari jana Novemba 12, Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa amesema kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo anaongeza muda wa kamati za rufani za wilaya wa kupokea, kusikiliza na kutoa uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa kwa muda wa siku mbili zaidi hadi Novemba 15, 2024.
Mamlaka hayo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 52 ya Tangazo la Serikali Na.571,573, 574 na Kanuni ya 50 ya Tangazo la Serikali Na.572 yote ya tarehe 12/7/2024.
“Hivyo, muda unaongezwa kutoka tarehe 13/11/2024 na sasa rufaa zitapokelewa, kusikilizwa na kutolewa uamuzi hadi tarehe 15/11/2024 saa 12 Jioni. Hivyo, wagombea wote ambao pingamizi zao hazikukubalika wanaweza kuwasilisha rufaa zao mpaka tarehe 15 Novemba, 2024,” amesema Mchengerwa.
Aidha, Mchengerwa amezielekeza kamati za rufani za wilaya kuitisha fomu za wagombea wote walioenguliwa na ambao hawakuteuliwa ili kufanya mapitio na kujiridhisha na sababu zilizosababisha wagombea hao kutoteuliwa ili haki iweze kutendeka kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.
Mchengerwa pia katika taarifa yake amewaelekeza wasimamizi wa uchaguzi katika halmashauri zote kuwarejesha wagombea wa vyama vyote ambao walienguliwa kwa sababu ya kutodhaminiwa na vyama vyao katika ngazi ya kijiji au mtaa licha ya kuwa vyama hivyo viliwasilisha barua za kuainisha ngazi ya chini ya udhamni kuwa ni kata.
Hata hivyo, Mchengerwa amevitaka vyama vya siasa ambavyo wagombea wao wameenguliwa kutumia vizuri muda huo wa siku mbili ulioongezwa kuhakikisha wanasimamia wagombea wao waweze kuwasilisha rufaa zao kwa kamati za rufani zilizopo katika kila wilaya husika akisisitiza ofisi yake itaendelea kusimamia misingi ya utawala bora.
“Ofisi ya Rais Tamisemi itaendelea kuhakikisha inasimamia misingi ya Utawala Bora ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka na kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi,” amesema Mchengerwa.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Neema kwa wagombea wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Tamisemi ikiongeza muda wa kukata rufaa
Arusha. Huenda wagombea wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 …..baada ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusogeza mbele muda wa kupitia fomu za maombi na kukata rufaa kwa walioenguliwa hadi Novemba 15 mwaka huu.
Kwa siku za hivi karibuni baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikitoa matamko ya kutoridhishwa na jinsi mchakato wa kuchukua fomu pamoja na kupitisha wagombea ulivyoendeshwa wakibainisha maelfu ya wagombea wao kukatwa majina pamoja na ufinyu wa muda uliotolewa kwa ajili ya zoezi hilo.
Taarifa ya Mohamed Mchengerwa Waziri wa Tamisemi iliyotolewa Novemba13, 2024 inafafanua kuwa maoni yaliyotolewa na wadau wa uchaguzi huo ikiwemo vyama vya siasa yameifanya wizara hiyo kusogeza mbele zoezi hilo hadi Novemba 15 mwaka huu.
“Muda unaongezwa kutoka tarehe 13/11/2024 na sasa rufaa zitapokelewa, kusikilizwa na kutolewa uamuzi hadi tarehe 15/11/2024 saa 12 Jioni. Hivyo, wagombea wote ambao pingamizi zao hazikukubalika wanaweza kuwasilisha rufaa zao mpaka tarehe 15 Novemba, 2024,”imesema taarifa ya Mchengerwa.
Ndani ya kipindi hicgo Mchengerwa ameagiza kamati za rufani za wilaya kuitisha fomu za wagombea wote walioenguliwa/hawakuteuliwa ili kufanya mapitio na kujiridhisha na sababu zilizopelekea wagombea hao kutoteuliwa ili haki iweze kutendeka kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.
“Ninawaelekeza wasimamizi wa uchaguzi katika halmashauri zote kuwarejesha wagombea wa vyama vyote ambao walienguliwa kwa sababu ya kutodhaminiwa na vyama vyao katika ngazi ya Kijiji/Mtaa…
…Pmoja na kuwa vyama hivyo viliwasilisha barua za kuainisha ngazi ya chini ya udhamni kuwa ni Kata ikiwemo Chama cha ACT-Wazalendo kilichowasilisha ngazi yake ya udhamini kuwa ni ngazi ya Kata,”ameongeza Mchengerwa.
Maagizo hayo ya Tamisemi yanaenda sambamba na kuvitaka vyama vya siasa ambavyo wagombea wao wameenguliwa kutumia vizuri muda wa siku mbili ulioongezwa kusimamia wagombea wao kuwasilisha rufaa zao kwa kamati za rufani zilizopo katika kila wilaya husika.
Katika hatua nyingine Tamisemi imesema itaendelea kuhakikisha inasimamia misingi ya Utawala Bora ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka na kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi.