Tunachokifahamu kuhusu ujenzi wa soko jipya la Kariakoo

April 15, 2023 8:04 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Hadi Februari mwaka huu Sh4.16 bilioni zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa soko la Kariakoo.
  • Ujenzi wa soko hilo umefikia hatua ya kumwaga jamvi la ghorofa ya tano kati ya ghorofa sita.
  • Litakamilika Oktoba 2023 na kuchukua wafanyabiashara 2,300. 

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki amesema hadi kufikia Februari mwaka huu Sh4.16 bilioni zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Serikali ilitoa Sh10 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kariakoo unaohusisha ujenzi wa jengo jipya na ukarabati wa jengo la soko la zamani lililoungua Julai 2021. 

“Hadi Februari, 2023, Sh4.16 bilioni zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu, sawa na asilimia 42 ya fedha zilizoidhinishwa,” amesema Kairuki wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2023/24 bungeni jijini Dodoma Aprili 14. 

Ujenzi wa soko hilo unaojengwa na kampuni ya Estim Construction Ltd umefikia hatua ya kumwaga jamvi la ghorofa ya tano kati ya ghorofa sita ikihusisha ghorofa mbili za chini ya ardhi (basement). 

Ukarabati wa jengo la zamani unaendelea na umefikia asilimia 62.

Soko Kuu la Kariakoo liliungua Julai 10, 2021 usiku huku  wafanyabaishara 224 wakipoteza bidhaa zao. Serikali haikuwaruhusu wafanyabiashara kurudi tena na badala yake ilianza mchakato wa ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa jengo la zamani. 


Soma zaidi:


Manufaa ya soko hilo

“Kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa soko hili kutachochea ukuaji wa biashara katika Jiji la Dar es Salaam, mikoa mingine na nchi jirani,” amesema Kairuki kuhusu soko hilo ambalo ni kiungo cha biashara Tanzania na nchi jirani. 

Ujenzi wa soko hilo unataraijwa kukamilika Oktoba, 2023 na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 2,300 sawa na ongezeko la wafanyabiashara 638 ukilinganisha na wafanyabiashara 1,662 waliokuwepo kabla ya ukarabati wa jengo la zamani na ujenzi wa jengo jipya. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV