TPA yaimarisha usafirishaji mizigo kwenda nje ya nchi

February 17, 2023 6:23 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni mizigo inayopitia katika bandari 16 za Ziwa Victoria.
  • Ni baada ya maboresho makubwa ya miundombinu ya usafirishaji.

Mwanza. Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) imesema imeimarisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa mizigo katika bandari zote 16 zilizopo ndani ya Ziwa Victoria baada ya kufanikiwa kuanza kusafirisha shehena za mizigo kwenda nchi jirani za Uganda na Kenya.

Meneja Bandari wa TPA, Ferdinand Nyati amesema mwaka 2022, wamefanikiwa kusafirisha mizigo 146,135 zaidi ya malengo iliyokuwa imejiwekea ya kusafirisha mizigo 98, 400.

Amesema hivi sasa wanapokea mizigo mikubwa ya sukari na mafuta ya kula kutoka Kisumu nchini Kenya na Uganda.

“Hivi sasa tunapokea mizigo mikubwa kutoka nchi za Uganda na Kenya, na kwamba pale itakapokapokamilika reli ya kisasa itasaidia kufungua ushoroba wa biashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kutumia reli na meli,” amesema Nyati akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha kamati ya maboresho ya bandari (PIC) kilichofanyika jijini Mwanza.

Amesema kwa sasa, TPA inaendelea kufanya maboresho ya miradi miwili mikubwa ambayo ni bandari ya Kemeondo na Bukoba ambayo itagharimu Sh20 bilioni na inatarajiwa kukamilika mwaka 2024.

Miradi mingine ambayo inatarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ununuzi wa taa za kuongozea meli zenye gharama ya Sh500 milioni, uendelezaji wa bandari kavu Fela Mwanza kwa awamu ya kwanza itakayogharimu Sh500 milioni na usimikaji wa taa za umemejua.

Akizungumzia suala la usafirishai, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL), Erick Hamissi amesema usafirishaji kwa njia ya reli na maji ni rahisi kwa kuwa unaokoa gharama za usafiri kuliko njia zingine kama ndege na magari.

Mkurugenzi huyo amesema huko nyuma wakati wanatumia meli ya Mv Umoja kusafirisha mizigo kwenda Uganda, mfanyabiashara mmoja amewahi kuokoa zaidi ya asilimia 42 ya fedha za usafirishaji wa mizigo kwa kutumia usafiri wa reli na meli.

“Tukimairisha usafiri kwa njia ya maji itashusha gharama za usafiri na kusaidia kuongeza mapato. Mathalan, tukipata tani milioni 3 takribani asilimia 50 ya mzigo inayotakiwa Uganda tunaweza kuona hata vitabu vya TRA vinashtuka,” amesema Hamissi.


Soma zaidi:


Kwa upande wake Anwari Mohamed anayemiliki bandari ya Nyehunge ameomba Serikali kuingilia kati suala la tozo zilizoelekezwa kwenye bandari hizo ambazo zipo hatarini kupoteza watumiaji wa usafiri huo hasa wa maisha duni.

“Hivi sasa tunashindwa kujua nani ni nani ambaye anapaswa kukusanya tozo za bandari kwa kuwa Tasac wanataka makusanyo lakini pia hivi sasa TRA nao wameleta notisi ya kuanza kukusanya mapato,” amesema Mohamed.

Awali, Mkurugenzi wa huduma za uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Aron Kisaka amesema suala la mgongano wa kimaslahi katika ukusanyaji wa mapato linapaswa kutatuliwa kwa mujibu wa sheria.

“Bandari zote ziwe binafsi au Serikali zinapaswa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, iwapo kuna changamoto yoyote ambayo mamlaka inaagizwa kutekeleza lakini ipo kinyume cha sheria iwasilishwe kwa mamlaka husika ili iweze kuangaliwa hayo mapungufu yanayosababisha wao wasitekeleze majukumu yao ipasavyo,” amesema Kisaka.

Kisaka pia ametumia fursa hiyo kuwataka wadau wa usafirishaji kuhakikisha wanalitangaza ziwa hilo na kutafuta mizigo inayopaswa kwenda nje ya nchi au kuingia ndani ya nchi ili wananchi waweze kuingiza mapato kutokana na biashara zitakazofanywa lakini pia bandari kuweza kuingiza mapato.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV