Tanzania yazidi kujiimarisha mapambano dhidi ya ujangili

December 8, 2022 1:17 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kupitia kutoa mafunzo kwa wenyeviti wa Kamati za Kanda za Kiikolojia za Kuratibu Doria (TCG’s)
  • Ripoti zinaonesha wanyama kuongezeka kutokana na kupungua kwa vitendo vya ujangili.

Dar es salaam. Ili kukomesha vitendo vya ujangili hapa nchini, Serikali imesema itaendelea kuongeza nguvu katika kuzuia na kupambana na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na biashara haramu ya nyara za Serikali.

John Ngowi, Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii amewaambia Wenyeviti wa Kamati za Kanda za Kiikolojia za Kuratibu Doria (TCG’s) kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mafunzo na doria. 

“Lengo la kutolewa kwa mafunzo haya ni kuharakisha na kuhakikisha majangili wote wanaokamatwa wanafikishwa mahakamani na mashauri yao yanaendeshwa kwa haraka na kwa ufanisi ili wahusika wapewe adhabu inayostahili kulingana na matakwa ya sheria za nchi yetu, “ amesema Ngowi.

Ngowi aliyekuwa akimwakilisha Mkurugenzi Msaidizi wa Uzuiaji Ujangili nchini katika  ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa TCG’s amesema mafunzo hayo yawasaidie kupanga mikakati endelevu ya kukomesha ujangili.


Soma Zaidi:

Mauaji ya mwanaharakati wa ujangili: 11 wahukumiwa kunyongwa hadi kufa


Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa sasa idadi ya wanyamapori imeongezeka katika Hifadhi za Taifa kutokana na jitihada mbalimbali za kukabiliana na ujangili ikiwemo doria.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana alipokuwa akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2022/23 alisema jumla siku doria 434,371 zimefanyika na kuwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 7,719 pamoja na nyara za Serikali na magogo yenye ujazo wa mita 1,218.

Meneja wa Mradi wa Kupambana na Ujangili na Usafirshaji haramu wa Nyara, Theotimos Rwegasira amesema mafunzo hayo yanatarajiwa kuleta mafanikio makubwa katika vita dhidi ya ujangili.

Mafunzo hayo yanayohitimishwa leo yamefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Duniani (UNDP) na Shirika la Mazingira (GEF) ili kuongeza juhudi za kukabiliana na ujangili.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV