Tanzania kuanza uhakiki wakimbizi kuimarisha usalama

January 22, 2024 11:28 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Rais Samia amesema uamuzi huo umekuja baada ya UNHCR ililokuwa likifanya kazi ya kurudisha wakimbizi katika nchi zao “kuishiwa nguvu”.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema itaanza uhakiki wa wakimbizi na waomba hifadhi kutoka nchi jirani ili kuwarejesha makwao wasiostahili na kuongeza usalama nchini.

Tanzania ni miongoni mwa nchi katika ukanda wa Afrika Mashariki zinazohifadhi kiwango kikubwa cha wakimbizi na waomba hifadhi kutoka nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) waliokimbia machafuko nchini mwao.

Katika hotuba yake leo Januari 22, 2024 jijini Dar es Salaam, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake itafanya uhakiki huo baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lililokuwa likifanya kazi ya kurudisha wakimbizi katika nchi zao “kuishiwa nguvu”.

“Tumefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na lile Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani lakini ukweli ni kwamba lile Shirika limeishiwa nguvu na ule moto wa kurudisha wakimbizi sasa umepungua,” amesema Rais Samia wakati wa mkutano wa saba wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) na makamanda.


Soma zaidi:Rais Samia awataka wanaoishi mabondeni kuhama kuepuka maafa


Rais Samia amebainisha kuwa baada ya zoezi la uhakiki Serikali itazungumza na nchi wanazotoka wakimbizi na waomba hifadhi hao ili kutafuta njia ya kuwarudisha.

“Kama mlivyosema wengine siyo wakimbizi wanaishi kama raia na wanajiona kama ni Watanzania kwa hiyo hili kama angalizo tumelichukua na tutakwenda kulifanyia kazi,” ameeleza Rais Samia.

Hata hivyo, Rais Samia hakuweka bayana uhakiki huo utaanza lini na zoezi la kuwarejesha litaanza lini. 

Miaka ya hivi karibuni Tanzania kwa kushirikiana na UNHCR imekuwa ikiwarejesha nyumbani wakimbizi wengi baada ya hali kwenye nchi zao kutulia. Hadi Mei 2023 wakimbizi 10,335 walirejeshwa makwao katika nchi za Burundi, Marekani, Canada, Ufaransa na Australia kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani. 

Kwa Mujibu wa  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda, Kuanzia Januari 1 hadi Disemba 31, 2023 Tanzania ilipokea waomba hifadhi 138,149 wanaotoka katika nchi za Rwanda, Burundi na DRC.

Jenerali Mkunda amewaambia wahudhuriaji wa mkutano huo kuwa baada ya kufanya mahojiano wamegundua kuwa baadhi ya waomba hifadhi, wamekimbia nchi zao kutokana na ugumu wa maisha na sio sababu za kiusalama kama walivyobainisha.

“Ni maoni yetu kwamba kuendelea kuwepo kwa wakimbizi hao na waomba hifadhi hao kwa muda mrefu ni tishio la usalama kwani kwa taarifa zilizopo ni kwamba baadhi ya waomba hifadhi  hao au wakimbizi au familia zao wameajiriwa serikalini kwa nafasi mbalimbali na wengine wamepewa teuzi kwa nafasi mbalimbali zenye maamuzi,” amesema Jenerali Mkunda.


Soma zaidi:Unavyoweza kuepuka ugonjwa wa ‘red eyes’


Jeshi kujiandaa kwa uchaguzi

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia ameliagiza Jeshi la Wananchi (JWTZ) na  vikosi vyote vya ulinzi na usalama nchini kujitayarisha kulinda usalama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge mwakani.

“Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba mwaka huu na mwakani tunaelekea kwenye chaguzi za nchi yetu na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi…

…kwa sababu tuko wengi, ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa kwa hiyo ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza,” amesema Rais Samia.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV