Tanzania, Ethiopia zafungua ukurasa mpya wa ushirikiano

January 25, 2021 12:26 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Zakubaliana kuimarisha uhusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na usafiri wa anga.
  • Shirika la Ndege la Ethiopia kutumika kuongeza idadi ya watalii Tanzania.
  • Wafungwa zaidi ya 1,000 ambao ni wahamiaji haramu kutoka Ethiopia wasamehewa bila masharti. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ethiopia, Sahle – Work Zewde  na kukubaliano mambo mbalimbali ikiwemo ukuzaji wa sekta ya mifugo na utalii ambazo zitazinufaisha nchi hizo mbili. 

Rais Magufuli aliyekua akizungumza leo Januari 25, 2021 wilayani Chato Mkoa wa Geita alipokutana na Zewde amesema ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia umeimarika na unaendelea kulinufaisha Taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara kati ya na uwekezaji.

“Katika Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimesajili miradi 13 kutoka Ethiopia yenye thamani ya Dola za Marekani 14.57 milioni (Sh33.8 bilioni) ambazo zimetoa ajira zipatazo 677,” amesema Dk Magufuli akibainisha kuwa,anawaalika wawekezaji wa Ethiopia kuja kuwekeza Tanzania ili kutumia rasilimali zilizopo. 

Amesema licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi barani Afrika bado haijanufaika, hivyo wawekezaji wa Ethiopia wanakaribishwa kuwekeza katika sekta ya mifugo ili kutengeneza fursa za ajira.

“Ethiopia imenufaika sana na soko la mifugo. Sisi mifugo yetu haijatupa faida kubwa kama wenzetu wa Ethiopia,” amesema Dk Magufuli baada ya kufanya mazungumzo na mgeni wake.

Licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi barani Afrika bado haijanufaika, hivyo wawekezaji wa Ethiopia wanakaribishwa kuwekeza katika sekta ya mifugo ili kutengeneza fursa za ajira. Picha| EATV.

Awasemehe wafungwa wa Ethiopia

Rais Magufuli amewasamehe wafungwa 1,789 ambao ni wahamiaji haramu kutoka nchi ya Ethiopia akisema ni ishara ya urafiki uliopo baina ya Tanzania na nchi hiyo. 

“Tumezungumza naye namna ya kupanga mbinu za kuweza kuwaruhusu warudi kwao. Sisi hatuna masharti yoyote kwa kuzingatia  undugu na urafiki uliopo kati ya nchi hizi mbili. Tunawaruhusu waondoke,” amesema Rais. 

Naye Rais Zewde amesema amefurahishwa na hatua hiyo, ambayo ni ishara ya urafiki uliokomaa baina ya Tanzania na Ethiopia huku akisema atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahamiaji wote wanarudishwa nyumbani na kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwaruhusu kurudi nchini kwao bila masharti yoyote.


Soma zaidi:


Utalii nao waongelewa

Kwa ngazi ya utalii, viongozi hao wamejadiliana kuona namna nchi hizo mbili zinaweza kunufaika na utalii hasa ikizingatiwa kuwa Ethiopia inafanya vizuri katika sekta ya usafiri wa anga.

Rais Magufuli amesema yeye pamoja na Rais Zewde wamefikia makubaliano ya matangazo ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini kati ya bodi ya utalii ya Tanzania (TTB) na Shirika la Ndege la Ethiopia, ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini. 

“Tunaamini tuwe na uhusiano ambao una mizizi imara kabisa na nchi ya Tanzania ndiyo maana jukumu la kwanza kabisa litakuwa ni kupitia makubaliano na mikataba yote iliyopo na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano,” amesema Rais Zewde.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...