TAA kukabidhiwa rasmi uwanja wa ndege KIA, Novemba 10, 2023

November 9, 2023 8:30 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya Bunge kuitaka Serikali kuja na kauli kuhusu uendeshaji wake.
  • Spika Tulia asema wanasubiri utekelezaji, ripoti kusomwa Februari 2024.

Dar es Salaam. Hatimaye, mara baada ya kubanwa mbavu na Bunge,Serikali imebainisha kuwa itakabidhi rasmi Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kesho Novemba 10, 2023.

Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa aliyekuwa akisoma taarifa ya wizara yake bungeni  leo Novemba 9, 2023 amewaambia wabunge kuwa wamechukua hatua hiyo kufuatia maagizo ya Bunge pamoja na kuisha kwa mkataba wa uendeshaji na ukodishaji.

“Serikali itakabidhi rasmi uwanja wa KIA kwa TAA kuanzia Novemba 10, 2023 kwa kuzingatia sheria, taratibu za Serikali na kama ilivyoelekezwa na Bunge,” amesema Profesa Mbarawa jijini Dodoma.

Mbarawa ameongeza kuwa mara baada ya makabidhiano, Serikali itaendelea kusimamia na kuratibu shughuli za uhamishaji ili kulinda maslahi ya Taifa.


Soma zaidi : Mambo muhimu ya kuzingatia unapokata rufaa ya mkopo HESLB 2023 – 24


Novemba 5, 2023 wakati wa kikao cha tano cha Bunge, Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson aliitaka Serikali kueleza sababu za kutokabidhi uwanja wa ndege wa KIA kwa TAA kama ambavyo iliazimiwa na Bunge mapema mwezi Februari 2023.

Baada ya kutoridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk. Eliezer Mbuki Feleshi na Profesa Mbarawa, Spika Tulia aliwapa muda wa kuja na kauli ya Serikali kuhusu jambo hilo kabla Bunge halijatoa uamuzi wake.

Awali uwanja wa KIA ulikuwa unaendeshwa na Kampuni ya Uendeshaji na Uendelezaji wa uwanja huo (KADCO) ambayo Serikali iliinunua mwaka 2011 na kuwa chini ya Serikali kwa asilimia 100.

Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa mkanganyiko wa uendeshaji wa uwanja huo ulitokana na uwepo wa sheria mbili tofauti zinazozimamia taasisi hizo, ingawa jambo hilo limekwisha patiwa ufumbuzi.


Soma zaidi : ‘Betting’, vinywaji baridi kuchangia bima ya afya kwa wote Tanzania


Spika anena

Pamoja na kuipongeza Serikali kwa kufanyia kazi maagizo ya Bunge kwa wakati Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson, amesema wanasubiri kuona utekelezaji wa jambo hilo ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu atawasilisha ripoti yake katika bunge lijalo.

“Bunge la Februari tutasikia jambo hili likiwa limekamilika, na Serikali kama kuna mambo mnatakiwa kuyafanya baada ya haya makabidhiano myatekeleze….

… Tutakapokuwa tunasikiliza taarifa ya kamati mwezi Februari basi tusikie uwanja wa KIA upo chini ya TAA na TAA wako pale,” amesema Spika Tulia huku akipigiwa makofi na wabunge.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV