Subaru, Toyota kuingiza sokoni magari ya umeme 2022

December 23, 2021 2:20 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Magari hayo yanakuja na mifumo miwili ya uendeshaji. 
  • Mfumo wa 2WD na 4WD na kila mfumo unauwezo wake wa betri.
  • Kati ya gari hizo, zipo zinazotumia mfumo wa umemejua.

Dar es Salaam. Kampuni za kutengeneza magari nchini Japan za Subaru na Toyota zinazotengeneza zimewapatia wadau wa mazingira cha kuongelea baada ya kutangaza kuingiza sokoni magari yake ya kwanza ambayo yanatumia umeme badala ya mafuta ya petroli.

Gari hizo zinajulikana kama “Solterra SUV” kutoka kwa Subaru na “BZ4X” kutoka kwa Toyota na zinatarajiwa kuingia sokoni kabla ya kuanzia mwaka 2022.

Kampuni hizo zenye miundo kadha wa kadha ya magari yanayotumia mafuta zimetoa matangazo hayo hivi karibuni baada ya kutoa picha za kuchokoza soko tangu mwezi Mei mwaka huu.

Picha hizo zililenga kutangaza ujio wa gari hayo. Kwa mujibu wa Shirika la Habari za teknolojia, The Verge, magari hayo yametengenezwa kwa kushirikiano wa kampuni hizo.

Gari ya Toyota inaambatana na mfumo wa umeme jua. Picha| Toyota.

Nini kipya kwa Subaru Solterra?

Gari hiyo inakuja na mifumo miwili. Mtu atachagua kununua Solterra yenye mfumo wa kuendesha matairi mawili (2WD) au ile yenye kuendesha matairi manne (4WD).

Kwa gari inayotumia umeme, uwekezaji mkubwa hufanyika kwenye betri ili liweze kutumika na mtumiaji bila presha ya gari kumzimikia njiani.

The Verge imeandika kuwa, betri ya Solterra 2WD itaweza kutimika kwa hadi Kilomita 530 huku betri ya 4WD ikitumika kwa hadi kilomita 460.

Kwa mujibu wa Subaru, betri likiisha, gari hiyo ina uwezo wa kuchajiwa kwa haraka (fast charging). Hata hivyo, Subaru haijatoa taarifa ya kuwa itachukua muda gani betri kujaa.


Soma zaidi


Hodi Hodi BZ4X

Gari hiyo licha ya kuwa na mfumo wa umeme wa jua kwa juu kama ilivyo gari mpya kutoka kampuni ya Tesla, Model S pia inatumia teknolojia mpya ya uskani ambao sio wa duara kama ilivyozoeleka. Ni uskani unaojulikana kama Steering Yoke.

Hata hivyo, BZ4X inakuja na mfumo wa “Steering wheel” ili kwa watu wasiopenda mfumo wa “yoke” warudi kwenye zama za awali.

Kwa gari ya umeme ya Toyota, uwezo wake wa betri ni mdogo kiasi ikilinganishwa na Subaru kwani Toyota ina uwezo wa betri wa kilomita 310 kwa “WD na kilomita 286 kwa 4WD kwa kila mzunguko mzima wa chaji.

BZ4X ina uwezo wa kuchajiwa na kujaa kwa hadi asilimia 80 ndani ya nusu saa.

Mfumo wa umeme jua unaoambatana na gari ya Toyota, una uwezo wa kuzalisha umeme unaotosha kusafiria hadi kilomita 1,800 kwa mwaka.

Ifikapo 2022 tunaenda wapi? Subaru au Toyota?

Gari aina ya Solterra 2WD iliyotengenezwa na kampuni ya Subaru ya Japan. Picha| Subaru.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW