Ni ushindani: Lexus kuingiza sokoni gari la umeme mwezi huu

April 7, 2022 9:41 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Gari mpya ya umeme ya Lexus RZ inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni. Picha| Lexus.


  • Inatarajiwa kutoka Aprili 20, 2022.
  • Kampuni hiyo ya Japan kuongeza ushindani kwa Tesla.
  • Gari hii ni mwanzo wa safari ya lexus kuwa kampuni ya magari ya umeme pekee.

Dar es Salaam. Tumeshasikia kutoka kwa Toyota, Subaru, Apple na Meredes Benz kuhusu ujio wa magari yanayotumia umeme kutoka kampuni hizo za zinazotengeneza magari duniani.

Kampuni ya magari ya Lexus ya nchini Japan imeingia katika ushindani wa kutengeneza magari ya umeme, ikiwa ni hatua ya kuboresha sekta ya usafiri dunia kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na kampuni mama ya Toyota imetangaza kuitambulisha gari yake ya umeme Jumatano ya Aprili 20 mwaka huu huku picha tangulizi za gari hilo zikionyesha teknolojia zinazoambatana na gari hiyo.

Moja wapo ya teknolojia iliyoonekana ni usukani wa “yoke” ambao huenda Lexus amejifunza kutoka kwa gari za umeme za kampuni ya Tesla.


Soma zaidi:


Wakati Toyota ikitangaza gari yake ya BZ4X iliainisha kuwa mtu ana uwezo wa kuchagua gari yake iwe na usukani wa kawaida au Yoke lakini Lexus haijaweka wazi kama mtumiaji atakuwa na uwanja wa kuchagua.

Gari hiyo iliyopewa jina la RZ 450e, huenda ikazinduliwa sambamba na gari nyingine kutoka kwa Lexus ambayo ina muundo sawa na ule wa BZ4X ya Toyota. 

Kwa wale wanaojua kilichopo kati ya Toyota Harrier na Lexus Harrier wanaweza kuelewa ninachozungumzia.

Ujio wa gari hiyo ya umeme, ni hatua za Lexus kuachana na magari ya petroli na kujikita katika utengenezaji wa magari ya umeme pekee ifikapo mwaka 2035.

Gari mpya ya umeme ya Lexus itakuja na maajabu yapi? Usikae mbali na ukurasa wa Nukta Habari upate mbivu na mbichi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV