Tanzania yaimarisha uchunguzi wa afya kukabiliana na Ebola

October 17, 2026 2:40 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kujaza fomu ya taarifa za afya za wasafiri pamoja na ufuatiliaji wa afya kwa siku 21.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imeimarisha hatua za uchunguzi wa afya katika mipaka ya nchi, viwanja vya ndege na bandari ili kudhibiti hatari ya kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Ebola (EVD).

Tanzania imechukua tahadhari hizo za kiafya kufuatia kuripotiwa kwa visa vitatu nchini Kenya takribani miezi mitano tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huo kwa mara ya kwanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Taarifa ya Dk Grace Magembe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya iliyotolewa  Oktoba 17, 2026, imesema hatua hizo zinalenga kuimarisha ulinzi wa afya ya umma kwa wasafiri wanaoingia nchini.

Kulingana na taarifa hiyo, wasafiri wote wanatakiwa kujaza kwa usahihi fomu ya ufuatiliaji wa afya ya wasafiri kupitia tovuti ya wizara ya afya (https://afyamsafiri.moh.go.tz)kabla ya kuanza safari ya kuelekea Tanzania au wanapowasili nchini.

“Wasafiri wanapaswa kuhifadhi msimbo wa QR au namba ya kumbukumbu watakayopata baada ya kujaza fomu hiyo, kwa ajili ya kuhakikiwa na maafisa wa afya bandarini au katika vituo vya kuingilia nchini wanapowasili,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo kwa lengo la kuimarisha hatua za kulinda afya ya umma zinazohusiana na safari za kimataifa.

Hatua hizi za wizara zimechukuliwa kwa kuzingatia Kanuni za Kimataifa za Afya (2005), kama zilivyorekebishwa mwaka 2024, pamoja na Sheria ya Afya ya Umma ya Tanzania ya mwaka 2009.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wasafiri wote watafanyiwa uchunguzi wa afya, ikiwemo kupimwa joto la mwili, katika viwanja vya ndege, mipaka ya nchi kavu na bandari.

Sanjari na hatua hilo, mtu atakayeshukiwa kuwa na dalili za Ebola au ugonjwa mwingine wa kuambukiza atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za kitaifa za uchunguzi na udhibiti wa magonjwa.

Aidha, wasafiri watapewa taarifa za afya na kushauriwa kufuatilia hali zao za kiafya. Wale watakaobaini dalili za Ebola au ugonjwa mwingine wa kuambukiza wanapaswa kutoa taarifa katika kituo cha afya kilicho karibu, kituo cha kuingilia nchini au kwa mamlaka husika kupitia namba ya simu isiyotozwa gharama 199 au barua pepe poe@afya.go.tz.

Serikali pia itafanya ufuatiliaji wa lazima wa afya ya wasafiri walio katika hatari kubwa kwa siku 21, kupitia ujumbe wa kiotomatiki wa kila siku au njia nyingine za mawasiliano. 

Tahadhari nyingine zilizotolewa

Wizara ya Afya imewataka wasafiri wote na waendeshaji wa vyombo vya usafiri kuzingatia hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi, zikiwemo, kunawa mikono kwa usahihi na kutumia vitakasa mikono pamoja na kuepuka migusano ya kimwili isiyo ya lazima.

Vile vile, kutoa taarifa mapema wanapoona dalili zinazoweza kuashiria Ebola au ugonjwa mwingine wa kuambukiza na kushirikiana na maafisa wa afya wakati wa uchunguzi na ufuatiliaji wa hali zao za kiafya.

Aidha, chombo chochote cha usafiri kitakachobainika kuwa kimechafuliwa na mtu anayeshukiwa kuwa na Ebola au ugonjwa mwingine wa kuambukiza, mzigo au mabaki ya mwili wa binadamu, kitafanyiwa usafishaji na uondoaji wa vimelea katika kituo cha kuingilia nchini ili kuzuia kuenea kwa maambukizi.

Serikali pia imewashauri wasafiri wanaoondoka Tanzania kuzingatia masharti ya kuingia katika nchi wanakoelekea au nchi watakazopitia kwa ajili ya kuunganisha safari.

Serikali imesisitiza kuwa tahadhari hizo zitaendelea kuhuishwa kulingana na mwenendo wa mlipuko na tathmini ya hatari ya maambukizi.

Takwimu zilizoripotiwa na Kituo cha Ulaya cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (ECDC) zinaonyesha kuwa hadi Oktoba 13, 2026, DRC ilikuwa imerekodi visa 9,277 vilivyothibitishwa na vifo 4,478 kutokana na mlipuko huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Nukta TV

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV