Simu mpya za Android kuzipiku iPhone kwa ubora?

September 19, 2022 11:38 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya Android kuingiza sokoni chipu mpya uendeshaji simu.
  • Chipu hiyo inatajwa kuwa na kasi na ufanisi mkubwa kuliko simu za iPhone.

Dar es Salaam. Huenda umekuwa ukichukulia poa matumizi ya simu zitumiazo mfumo wa endeshi wa Android, lakini kwa siku chache zijazo huenda simu zake zitakuwa na ufanisi mkubwa kuliko simu mpya za iPhone 14.

Shirika la uundaji programu na huduma za teknolojia la Qualcomm la Marekani linatarajiwa kufanya mkutano wake kati ya Novemba 15 na17, 2022 ili kuzindua chipu mpya ya Snapdragon 8 Gen 2 inayotarajiwa kuzidi ubora wa utendaji na kasi ya chipu zinazotimiwa sasa na kampuni ya Apple.  

Taarifa iliyochapichishwa kupitia mtandao wa androidcentral inatoa maelezo kuhusu chipu mpya ya Snapdragon 8 Gen 2, ikisema kwamba “tunaweza kuona toleo la “masafa ya juu zaidi” la chipu mpya mwaka wa 2023.”

Inaonekana, chipu hii inaweza kufikia kasi ya masafa ya 3.4-3.5GHz. Kwa kulinganisha, hii itakuwa juu kidogo kuliko Snapdragon 8+ Gen 1 inayotumika kwenye baadhi ya simu bora zaidi za Android leo, zikitumia masafa ya 3.2GHz.

Chapisho hilo pia linapendekeza kuwa chipu mpya inaweza kupokea ongezeko la kitengo cha usindikaji wa picha (GPU) na kwamba nguvu ya ajabu ya GPU ya chipu hiyo inaweza kushinda nguvu ya chipu mpya ya A16 Bionic kutoka Apple.  


soma pia

Kumbuka kwamba utendaji mahiri wa simu unategemea mambo mengi, siyo tu kasi ghafi ya chipu inayoendesha kila kitu. Ufanisi wa usimbaji wa programu, kiasi cha RAM inayopatikana na usimamizi wa halijoto ya simu.

Tofauti na mfumo wa Android, Apple inasimamia mchakato wake mzima wa ubunifu wa programu zenye kasi na maunzi (hardware) zinazotumika kwenye simu zake, bila kutegemea watengeneza chipu wengine.

Mabadiliko hayo mapya yatashuhudiwa mapema kwenye simu za Samsung Galaxy S22, Samsung Galaxy Z Fold 4, Xiaomi 12 Pro, OnePlus 10 Pro, Sony Xperia 1 IV na zaidi zinazotumia Snapdragon 8 Gen 1.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.