Serikali yaruhusu uwekezaji kwa wakazi wa Ngorongoro waliohamishiwa Msomera

January 17, 2024 12:53 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yawakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
  • Yasema kijiji cha Msomera kinaweza kuendelezwa na kufungua ajira. 
  • Waliohama kwa hiari wafikia 3,822.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imefungua milango ya fursa za uwekezaji katika kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, ili kuboresha maisha ya wakazi wa Ngorongoro waliohamia katika kijiji hicho.

Zoezi la kuwahamisha wakazi wa Ngorongoro katika kijiji cha Msomera lilianza Juni 2022 lengo likiwa ni kulinda ekolojia ya hifadhi hiyo ya Taifa itayotajwa kuwa miongoni wa vivutio vya utalii vikubwa Afrika Mashariki.

Ili kutekeleza zoezi hilo Serikali ilitenga Sh700 bilioni iliyowezesha ujenzi wa nyumba za vyumba vitano kila moja, kuwalipa wakazi hao fidia na kujenga miundombinu mingine itakayowawezesha kuishi katika kijiji hicho.

Msemaji  Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi aliyekuwa akizungumza katika mkutano na wanahabari uliofanyika jijini Tanga, Januari 17, 2023 amesema baada ya awamu kadhaa za kuhamisha wakazi hao hivi sasa Msomera ipo wazi kwa uwekezajii.

“Hakuna ugumu wowote wa muwekezaji kufika katika eneo lolote la nchi yetu ilimradi anafuata taratibu, wawekezaji wa nje na  wa ndani wanaruhusiwa kufika kama ilivyo katika maeneo mengine…

“…Ni wao tu kuchangamka au wananchi wenyewe wa hapa kuchagamka. Serikali inachofanya ni kuweka vivutio ili mwekezaji aweze kufika,” amesema Matinyi.


Zinazohusiana:Idadi wanaondoka Ngorongoro yazidi kuongezeka


Msemaji huyo amebainisha kuwa miongoni mwa shughuli za uwekezaji zinazoweza kuanzishwa katika kijiji hicho ni ujenzi wa maduka, sehemu za burudani na viwanja vya michezo ambazo zote zinawezekana kutokana na  ukubwa wa eneo hilo.

Kufunguliwa kwa fursa hiyo ya uwekezaji Msomera kunatoa nafasi kwa wakazi wa kijiji hicho waliohamishwa kutoka hifadhi ya Ngorongoro ambayo kisheria haikuruhusu uwekezaji kuishi maisha ya kisasa tofauti na ya wali.

Kwa mujibu wa Matinyi mpaka sasa jumla ya kaya 677 zenye watu 3,822 na mifugo 18,102 zimehama kwa hiari kutoka hifadhi ya Ngorongoro na kuhamia katika kijiji cha Msomera.

Idadi hiyo ya kaya zilizohamia Msomera ni sawa na asilimia 0.3 ya lengo la Serikali la kuhamisha kaya 22,000 zilizopo Ngorongoro.

Ili kuboresha maisha ya wakazi hao, Matinyi ameeleza kuwa  Serikali inaendelea kuboresha miundombinu mingine katika kijiji hicho ikiwemo ujenzi wa hospitali, madarasa, barabara, mnada, malisho ya mifugo, vituo vya kuuza maziwa pamoja na miundombinu ya mawasiliano.

/
No matches found for this filter
22 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
23 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

Nukta TV