Serikali yajifunga kitanzi ujenzi vituo 77 vya polisi Tanzania

August 3, 2024 2:21 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni vile ambavyo ujenzi wake ulianzishwa na wananchi hadi kwenye ngazi ya boma.
  • Yajipanga kujenga vituo vingine 12 vipya vya polisi katika maeneo mbalimbali nchini.

Mwanza. Serikali ya Tanzania imesema itakamilisha ujenzi wa vituo vya polisi 77 vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi huku ikilenga kujenga vituo vingine vipya 12 nchini ili kusogeza huduma karibu na jamii na kutokomeza uhalifu.

 Ukosefu wa vituo vya polisi jirani na makazi ya watu ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili baadhi ya maeneo nchini kiasi cha kupunguza kiwango cha usalama na kuongeza gharama kwa wananchi kuzifuata huduma hizo umbali mrefu. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amewaambia wakazi wa Jiji la Mwanza leo kuwa Serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi wa vituo hivyo ambavyo ujenzi wake ulianzishwa kwa nguvu za wananchi katika mwaka huu wa fedha wa 2024/25.

 “Mbali na kukamilisha ujenzi wa vituo hivyo pia katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali itajenga vituo vingine vipya 12 kwenye kata mbalimbali pamoja na nyumba za askari wa Jeshi la Polisi kwa kutumia fedha za mfuko wa tuzo na tozo,” amesema Sillo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya polisi vya Buswelu na Nyegezi jijini Mwanza. 

Polisi ni miongoni mwa wafanyakazi wanaokabiliwa na uhaba wa nyumba za watumishi kiasi cha kuwafanya kuishi nje maeneo yao ya kazi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo akiwa na viongozi wengine wa Jeshi la Polisi baada ya kutembelea Zahanati ya Mabatini inayotumiwa na Askari wa Jeshi la Polisi jijini Mwanza. Picha Mariam John/Nukta

Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza walieleza kuwa kutokana na umuhimu wa huduma za polisi hususan kukabiliana na uhalifu, wananchi walijitoa kwa michango na nguvu kazi kujenga vituo hivyo hadi kufikia hatua ya boma ila sasa wana wasiwasi havitamalizwa kwa wakati.

Diwani wa Kata ya Nyegezi, Edith Mudogo ameiomba Serikali kuweka fedha ili kuharakisha ujenzi wa kituo chao cha polisi ili waweze kupata huduma za kijamii za polisi kama maeneo mengine nchini.

“Tumeanza taratibu kwa kupiga mawe hadi kufikia hatua hii hivyo tunaiomba Serikali ione umuhimu wa kuongeza nguvu zaidi ujenzi ukamilike ili tupate huduma kwenye ukanda huu wa Nyegezi,” amesema Mudogo. 

Katika ziara yake, Sillo pia ametembelea zahanati ya Jeshi la Polisi Mabatini iliyopo Kata ya Mabatini inayotumiwa na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza na wananchi na kubaini kuwa kwa sasa inakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba pamoja na wodi ya wanaume.

 Kiongozi huyo aliahidi kuiingiza zahanati hiyo kwenye mipango ya maboresho kupitia wizara hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula amesema zahanati hiyo ya mabatini ina uhitaji mkubwa wa vifaa tiba na mashine mbalimbali za kufanyia vipimo vya kiafya hivyo ameiomba Serikali kuhakikisha wanakifanyia marekebisho makubwa maana kinatumika kama Zahanati ya Kanda ya Ziwa.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV