Serikali yafuta maonyesho ya nane nane mwaka 2021

February 10, 2021 11:24 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Sherehe hizo zilizokuwa zifanyike mwezi Agosti, 2021 katika kanda nane katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.
  • Fedha zilizotengwa kwa ajili shughuli hiyo zitatumika kuimarisha huduma za ugani ili kuleta mapinduzi ya kilimo. 
  • Serikali kufanya tathmini ya ufanisi ya maonyesho hayo miaka ijayo. 

Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo Prof Adolf Mkenda ametangaza kufutwa kwa sherehe za maonyesho ya wakulima maarufu kama Nane Nane kwa mwaka 2021 na fedha zilizotengwa kwa ajili shughuli hiyo zitatumika kuimarisha sekta ya kilimo.  

Sherehe hizo zilitakuwa zifanyike mwezi Agosti, 2021 katika kanda nane katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Prof Mkenda amesema Serikali inakusudia fedha zote za umma zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe hizo zitumike kuimarisha huduma za ugani nchini.

“Shughuli zote za Nanenane mwaka huu zimefutwa rasmi na Serikali. Hhivyo fedha zote zilizotengwa kwa kazi hiyo zitatumika kuboresha huduma za ugani nchini ili kuleta mapinduzi ya kilimo,” amesema waziri huyo leo (Februari 10, 2021) Jijini Dodoma mbele ya  waandishi wa habari.

Amesema shughuli za Nane Nane lazima ziendane na upatikanaji wa huduma bora za ugani kuinua sekta ya kilimo, hivyo Serikali lazima ijipange vema.


Zinahusiana: 


Kufuatia uamuzi huo wa Serikali, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau itatumia muda huo kufanya tathmini ya namna maonyesho ya Nane Nane yamekuwa yakifanyika na kuona maeneo ya kuboresha  ili yawe na tija katika kukuza sekta ya kilimo na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa ujumla. 

Aidha, Prof Mkenda amesema wizara yake itaunda kikosi kazi maalum kwa ajili ya kufanya tathmini hiyo ili kilete mapendekezo yatakayokuwa na tija katika maadhimisho ya Nane Nane katika miaka ijayo.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV