Ahueni: Bei ya mbolea kushuka, Serikali ikitoa ruzuku ya pembejeo

August 8, 2022 4:12 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya Serikali kutoa ruzuku ya pembejeo.
  • Rais Samia aagiza ianze kutolewa Agosti 15.

Dar es Salaam. Huenda maadhimisho ya Nane Nane ya mwaka huu yatawapatia wakulima matumaini mapya katika msimu mpya wa kilimo baada ya Serikali kuzindua mpango wa ruzuku kwa pembejeo ikiwemo 

Hatua hiyo itapunguzia wakulima walizokuwa wakitumia awali kupata pembejeo za kilimo, jambo linaloweza kuongeza uzalishaji na masoko ya kilimo.

Akizungungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika mkoani Mbeya leo Agosti 8 wakati wa kilele cha sherehe za Wakulima Nane Nane, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema mpango huo unalenga kuwaondolea mzigo  wakulima  kutokana na changamoto za bei za mbolea.

Amesema kupitia mpango huo mbolea zote za kupandia zinazofahamika kama NPK zilizokuwa zikiuzwa kwa Sh122, 695 zitauzwa kwa Sh70 000 huku ruzuku ya Serikali ikiwa Sh52,695.

“UREA (ya kukuzia) itatoka Sh124,734 wakulima wataenda kuinunua kwa Sh70,000,” amesema Bashe.

Ili kunufaika na mpango huo wakulima wanatakiwa kuandikishwa na kuhakikisha wananunua pembejeo hizo kwa bei elekezi.

Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho ya Nanenane ambayo yamefanyika  kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale jijini humo, ameagiza ameagiza mpango huo wa ruzuku ya pembejeo kuanza Agosti 15  ili kuwawezesha wakulima kujipanga na msimu mpya wa kilimo.

‘’Waziri wa fedha umeniambia fedha ziko tayari ila kuna taratibu zinatakiwa zitimie, lakini nataka niseme kwamba ruzuku hizi zianze kuanzia Agosti 15 ili wakulima wajitayarishe kuanza msimu unaokuja,” amesema Rais Samia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane Kitaifa ambayo imefanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya Agosti 8, 2022. Picha| Ikulu.

Rais Samia atoa maagizo

Katika maadhimisho hayo Rais Samia ametaka kila mkoa kuhakikisha wanatenga eneo kwa ajili ya kilimo cha mashamba makubwa pamoja na kujikita kwenye kilimo cha biashara ili kukuza uchumi wa nchi.

“Kila mkoa upange eneo kubwa kwa lile zao ambao kwa mkoa ule litamea  vizuri na kuzalishwa jwa tija, “amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema Serikali imejipanga kuwawezesha vijana kujiingiza kwenye kilimo ambapo watapewa hati na kuunganishwa kwenye mikopo rahisi isiyo na riba kubwa.

“Niwaombe vijana ingieni kwenye shughuli  hii ya kilimo,” amesema Rais.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV