Serikali ya Tanzania yapendekeza kuwalipa posho watendaji wa kata, tarafa

June 10, 2021 3:16 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Madiwani wao wataanza kupatiwa posho zao kwenye akaunti ili kuwaondolea usumbufu na kuongeza ufanisi kazini.

Mwanza. Serikali inapendekeza kuanza kuwalipa madiwani posho zao kwenye akaunti zao kuanzia  mwaka wa fedha 2021/22 ili kuondoa usumbufu unaojitokeza na kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kila siku.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mwingulu Nchemba ameliambia Bunge jijini Dodoma leo Juni 10 kuwa kilio cha madiwani hao kimesikika na wamekuwa wakifanya kazi kwa wakati mgumu kiasi cha kuwakosesha ufanisi kazini. 

Amesema kilio cha viongozi hao wa Serikali za mitaa kimesikiwa na sasa Serikali kuu imependekeza kuanzia mwaka wa fedha 2021/22 madiwani hao wataanza kulipwa posho  zao kupitia  kwenye akaunti zao.

Katika maboresho hayo ya posho, Dk Nchemba aliyekuwa akisoma makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/22, amesema kuwa maofisa tarafa nao watapatiwa posho ya Sh100,000 kwa mwezi.

Waziri Nchemba amesema kumekuwepo na kilio cha maofisa tarafa kukosa posho kwa ajili ya kununulia mafuta kwenye pikipiki zao na kueleza kuwa kuwa kilio hiki kimesikiwa.

“Serikali inapendekeza kuanzia mwaka 2021/22, kuanza kulipa posho ya madaraka ya Sh100,000 kwa mwezi kwa kila Mtendaji Kata kupitia mapato ya ndani ya halmashauri yaliyokuwa yakitumika kulipa madiwani,” amesema.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV