Wabunge, mawaziri wenye madeni taasisi za Serikali kikaangoni
- Ni wale waliokopa na kushindwa kufanya marejesho hadi kufikia Juni 2022.
- Wakingiwa kifua majina yao yasitajwe.
Dar es Salaam.Spika wa Bunge la Tanzania Dk.Tulia Ackson, amewataka wabunge na mawaziri wenye madeni katika mashirika na taasisi za Serikali kurudisha mara moja fedha hizo kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhiidi yao.
Agizo hilo la Spika Tulia, linawahusu wabunge na mawaziri ambao walikopa na fedha au huduma katika mashirika ya Serikali na hawajalipa madeni hayo hadi kufikia Juni 2022.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) miongoni mwa mashirika ya umma yanayowadai wabunge na mawaziri ni pamoja na Kampuni ya mafuta ya (Tanoil) na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF).
Ripoti ya CAG, kwa mwaka 2021/22 imebaini uwepo wa mikopo wa Sh21.3 kwenye mfuko wa AGITF ambayo haijakusanywa na hivyo kuashiria upotevu wa fedha za umma.
Kwa upande wa Tanoil, ripoti ya CAG inaweka wazi kuwa kwa mwaka 2021/2022 iltengeneza hasara ya Sh7.8 kutokana na sababu mbalimbali ikkwemo kuuza mafuta kwa kampuni za ndani kwa bei ya chini kushinda ile iliyoelekezwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Soma zaidi:Mapato yasiyokusanywa Serikali za mitaa yaongezeka kwa asilimia 61.7
Wadaiwa wafichwa
Dk. Tulia, aliyekuwa akihitimisha uwasilishaji wa taarifa za kamati za Bunge zilizochambua ripoti tatu za CAG leo Novemba 4, 2023 amesema hatataja majina ya viongozi hao ili kulinda maslahi ya kibiashhara lakini wanatakiwa kurudisha fedha hizo kwa haraka.
“Siyataji tu majina yao kwa ajili ya kulinda maslahi yao ya kibiashara…wasinifikishe mahali ambapo nitaaanza mimi kuilipa Serikali kutumia pesa zao,”amesema Tulia.
Aidha, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga pamoja na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe nao wamewakingia kifua baadhi ya wabunge na mawaziri ambao majina yao yaliwasiishwa kwa Dk Tulia kuhusika katika ukopaji wa mikopo katika mashirika ya Serikali.
Kwa mujibu wa viongozi hao, mikataba ya biashara iliyoingiwa wakati wa ukopaji wa ikopo hiyo ni ya siri hivyo kusoma majina yao hadharani kutaingilia maslahi yao ya kibiashara na kuvunja makubaliano ambayo wameyaingia.
Leo Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Serikali Kuu na Mashirika ya Umma(PAC) pamoja na Uwekezaji wa Mitaji ya Uma (PIC) zimehitimisha uwasilishhwaji wa taarifa na utolewaji wa mapendekezo yao kuhusu ripoti ya CAG ya mwaka 2021/2022.
Miongoni mwa mapendekezo yaliyoibuliwa na kamati hizo ni pamoja na Serikali kuwachukulia hatua wote waliotajwa kushiriki ubadhirifu wa fedha za Umma kama walivyobainishwa katika ripoti ya CAG.
Mengine ni Serikali kulipa madeni yanayodaiwa na baadhi ya mashirika ya umma ikiwem Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Dawasa), o Suma JKT pamoja na Bohari ya Dawa (Msd).
Latest