Serikali kufuta kodi ya dhahabu inayouzwa Benki Kuu

June 14, 2024 7:07 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Lengo ni kuongeza akiba ya nchi ya fedha za kigeni na kupunguza tatizo la uhaba wa dola za Marekani. 
  • Pia itachochea ukuaji wa viwanda vya kusafisha madini (refineries) nchini.

Dar es Salaam. Huenda wachimbaji na wafanyabiashara wa dhahabu  watapata tabasamu baada ya Serikali kupendekeza kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya kiwango cha asilimia 0 kwa madini hayo yatakayouzwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania imeanzisha utaratibu wa kununua dhahabu kwa ajili ya akiba ya Taifa (National Gold Reserve) kwa lengo la kuimarisha akiba ya fedha za kigeni na kusaidia katika utekelezaji wa Sera ya Fedha.

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema hatua hiyo itahamasisha uuzaji wa dhahabu kwa BoT, na hivyo kuongeza akiba ya nchi ya fedha za kigeni na kupunguza tatizo la uhaba wa dola za Marekani. 

“Hatua hii inalenga pia kuchochea ukuaji wa viwanda vya kusafisha madini (refineries) nchini kwa kuwa Benki Kuu ya Tanzania hununua dhahabu baada ya kusafishwa na viwanda hivyo pekee,” amesema Mwigulu wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali Kuu kwa mwaka wa fedha wa 2024/25 leo Juni 13, 2024 bungeni jijini Dodoma.

Serikali pia imependekeza kutoza VAT kwa kiwango cha asilimia 0 kwenye madini ya dhahabu yatakayouzwa kwa viwanda vya kusafishia dhahabu nchini (refineries). 


Soma zaidi: Bajeti ya Serikali Tanzania yapaa hadi Sh49.35 trilioni


Waziri Mwigulu amesema hatua hiyo itachochea ukuaji wa viwanda hivyo nchini kwa kuhakikisha kuwa vinapata malighafi za kutosha (feed stock). 

“Pendekezo hili pia linalenga kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha kuwa madini ghafi ya dhahabu yanasafishwa nchini na kuongezewa thamani kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi,” amesisitiza waziri huyo mbele ya wabunge. 

Hadi Aprili 2024, BoT imenunua dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani milioni 26 (Sh67.8 bilioni) ambapo malengo ya Serikali ni kununua tani sita za dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani milioni 400 (Sh1.1 trilioni). 

Mwigulu amesema Serikali inaendelea kuhamasisha viwanda vya ndani vya kuchenjua dhahabu kufanya taratibu za kupata Ithibati ya Chama cha Soko la London la Madini ya Thamani (LBMA) ili kuwezesha dhahabu inayosafishwa kutambuliwa kwenye masoko ya kimataifa na kuweza kununuliwa kwa ajili ya kuhifadhiwa kama fedha.

Pendekezo lingine ni kufuta msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani kwenye madini ya thamani, madini ya vito na madini mengine ya thamani yanayouzwa kwenye vituo vya kusafishia dhahabu (refineries) vilivyopo nchini.

Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh18.2 bilioni.

Serikali inakusudia kutoza kodi ya zuio kwa kiwango cha asilimia mbili kwenye malipo yanayotokana na ununuzi wa madini ya viwandani (industrial minerals).

“Utozaji huu hautahusisha chumvi, madini ya metaliki au madini mengine ya thamani kama yalivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Madini, sura 123 yatakayouzwa na mmiliki wa leseni ya uchimbaji mdogo wa madini (Primary Mining Licence) au mchimbaji mdogo wa madini (Artisanal Miner),” amesema Mwigulu.  

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV