Serikali kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo Tanzania

August 8, 2025 4:56 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link

Arusha, Serikali ya Tanzania imejipanga kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo ili kuongeza mchango wake katika pato la Taifa na tija kwa wakulima wanaotegemea shughuli hiyo kijiingizia kipato.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza katika hafla ya kufunga maonesho ya nanenane kitaifa jijini Dodoma leo Agosti 8, 2025 amesema kuwa mkakati wa Serikali yake ni kuimarisha sekta hiyo na kutatua changamoto zote zinazoikabili.

“Kuptia agenda 10/30 tunalenga kuongeza kasi ya sekta ya akilimo hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka ili kuwainua watanzania wengi wanaotegemea sektahii…

…ahadi yetu yetu ni kuwa tutaendelea kuboresha sekta ya kilimo kwa mujibu wa changamoto zilizopo, tutaendelea kuimaisha matumizi ya dhana za kilimo na Tehama ili kuongeza tija zaidi kwa sababu tija katika kilimo ndyo tija kwa Taifa,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo ikiwa tayari Serikali imepiga hatua kadhaa katika kuboresha sekta hiyo ikiwemo ujenzi wa mabwawa na miundombinu ya umwagiliaji maji, utoaji wa mitaji kwa wakulima yenye riba nafuu, utoaji wa ruzuku, uongezaji wa thamani wa bidhaa na  kufungua masoko ya bidhaa za kilimo.

Mwaka 2024 sekta hiyo ilikuwa kwa asilimia nne na kuchangia asilimia 26.3 kwenye pato la Taifa na iliajiri asilimia 61.4 ya Watanzania, ilichangia kwenye usalama wa chakula kwa aslimia 128, ikitarajiwa kuongezeka maradufu hadi kufikia mwaka 2030.

Ili kuendelea kukuza sekta hiyo Rais Samia amewasisitiza wakandarasi kujenga miundominu hiyo kwa viwango stahiki huku akiwataka wananchi kuitunza ili iweze kutumika kwa muda mrefu zaidi.

“Niwaombe sana wakulima hubeba jukumu la kuendeleza na kutunza miundombinu panapong’oka basi patengenezwe haraka kinachoharibika kitengenezwe kwa haraka  ili wananchi walio wengi wanufaike na miundombinu hii,” amesema Rais Samia.

Pamoja na hayo Rais Samia amesema Serikali inajipanga kuimarisha upatikanaji wa mbolea na mbegu bora nchini ambapo kufikia mwaka 2030 mbegu zote zinazotumika nchini zitakuwa zinazalishwa nchini.

Rais Samia amesema kwa sasa upatinaji wa mbegu bora umeongezeka kutoka tani 44,581 mwaka 2021 hadi tani 97, 700 mwaka 2024.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.