Sababu za lifti za majengo marefu kuwa na vioo

November 8, 2019 9:34 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link

Sababu kubwa ya kwanini lifti nyingi hua na vioo ndani ni kumchangamsha mtu anapokuwa kwenye lifti. Picha | Mtandao.


  • Vinamchangamsha mtu anapokuwa kwenye lifti
  • Vioo hufanya chumba kuonekana kikubwa zaidi na kumpa uhuru aliyepo ndani.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatembelea au kufanya kazi katika majengo marefu ya ofisi au makazi ya kuishi, basi lifti (Elevators) siyo jambo geni kwako. 

Lifti hizo zina kazi kubwa ya kuwabeba na kuwarahisishia watu kupanda ngazi za maghorofa, jambo linaloweza kuchukua muda mrefu na hata kusababisha uchovu. 

Lakini bado utakuwa una maswali lukuki juu ya mandhari ya ndani ya lifti hizo ambazo ni angavu zinazomuwezesha mtu aliyepanda kujiona katika pande zote. 

Zingine zimewekwa vioo na spika za muziki. Lakini ni sababu gani zinazofanya watengenezaji wa lifti waweke vioo angavu ambavyo watu wanajiona? 

 Kwa mujibu wa tovuti ya Useless Daily imeeleza kuwa ni kumchangamsha mtu anapokuwa kwenye lifti kwasababu kwa kawaida binadamu anapokuwa kwenye hali ya kukosa kitu cha kufikiri kwa muda mrefu anakosa uchangamfu.

Hivyo, uwepo wa vioo ndani ya lifti humsaidia mtu kuchangamka na kuepukana na hali ya upweke.


Zinazohusiana:


Pia vioo hufanya chumba cha lifti kionekana kikubwa zaidi. Kwa kawaida chumba hicho ni kidogo kisichoweza kubeba watu wengi, hivyo kwa uwepo wa vioo hivyo husaidia chumba kuonekana kikubwa na kuwapa uhuru waliopanda. 

Ni fursa ya kujua kila kitu kinachoendelea unapokuwa kwenye lifti ikiwemo kujua ghorofa zinavyoenda mpaka kufika ghorofa unayoenda. Ni rahisi mtu kuona namba kupitia vioo kwa zile lifti zisizokuwa na sauti ya kuelezea namna ghorofa zinavyoenda. 

Mtumiaji mzuri wa teknolojia hii ya lifti katika majengo marefu, Julius Moshiro anasema amewahi kufikiria hali hiyo na kujiuliza na kujijibu kwa namna anavyofikiri yeye,

“Mi nafikiri huwa hivi vioo vipo kwa sababu muda mwingine mtu unaweza kuingia kwenye lifti ukageukia nyuma usiweze kuona namba, lakini kwa uwepo wa vioo hivyo, hata ukigeukia nyuma unaweza kuona kinachoendelea mbele,” amesema Moshiro.

Tuambie wewe, unafikiri nini kuhusu vioo vilivyopo kwenye lifti.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI, WIZARA YA MADINI IKIWASILISHWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI, WIZARA YA MADINI IKIWASILISHWA BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Nukta Africa kuzindua Nukta AI, siku ya uhuru wa vyombo vya habari

Nukta Africa kuzindua Nukta AI, siku ya uhuru wa vyombo vya habari

Nukta TV