Brela yatangaza mfumo mpya utoaji huduma leseni kundi ‘A’ 

April 24, 2026 5:55 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Sasa huduma zitapatikana kupitia mfumo wake wa ndani wa BRELA Online Services (BOS)
  • Maombi yote ya leseni yaliyowasilishwa kupitia mfumo wa TNBP kabla ya Aprili 19, 2026 yanapaswa kukamilishwa kupitia mfumo huo kabla ya Mei 1, 2026.

Dar es Salaam. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) umetangaza kuhamishia huduma zote za leseni Kundi ‘A’ kwenda kwenye mfumo mpya wa BRELA Online Services (BOS), hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wafanyabiashara.

Kwa mujibu Brela, huduma hizo ambazo awali zilikuwa zinapatikana kupitia mfumo wa Tanzania National Business Portal (TNBP) ni pamoja na utoaji wa leseni mpya za biashara, uhuishaji wa leseni, utoaji wa leseni za matawi, mabadiliko ya anuani za biashara pamoja na kusitisha leseni za biashara.

Hata hivyo, Brela imesema mbali na kuhamisha huduma hizo imeongoza huduma mpya kwenye mfumo wa BOS, ikiwemo huduma ya utafutaji wa taarifa za leseni za biashara pamoja na kufanya maombi ya leseni mpya ya biashara kupitia leseni ambayo tayari mwombaji anayo.

Ni kwa wamiliki wa leseni kundi ‘A’ pekee

Mabadiliko haya ya utoaji huduma yanawahusu wamiliki wa leseni ya kundi ‘A’ pekee inayotolewa na Brela na si kundi ‘B’ ambayo hutolewa na halmashauri.

Leseni kundi ‘A’ ni leseni inayotolewa kwa biashara kubwa na za kimkakati kama vile viwanda, makampuni ya huduma na uwekezaji mkubwa, huku Kundi ‘B’ zikihusisha zaidi biashara ndogo na za kati zinazofanyika ndani ya mipaka ya halmashauri husika.

Umiliki wa leseni ya kundi ‘A’ humpa mfanyabiashara uwezo mkubwa wa kiutendaji, ikiwemo uwezo wa kushiriki kikamilifu katika zabuni za Serikali na taasisi binafsi, kupata urahisi wa kufikia mikopo kutoka taasisi za kifedha, pamoja na kuongeza uaminifu kwa wawekezaji na washirika wa biashara ndani na nje ya nchi. 

Wamiliki wa biashara kujisajili upya

Kwa sasa, wadau wote wanaokusudia kuwasilisha maombi mapya au huduma zilizoorodheshwa wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia tovuti ya mfumo wa BOS

Hata hivyo, Brela imeelekeza kuwa maombi yote ya leseni yaliyowasilishwa kupitia mfumo wa TNBP kabla ya Aprili 19, 2026 yanapaswa kukamilishwa kupitia mfumo kabla ya Mei 1, 2026.

Kwa upande wa watumiaji, wamiliki wa kampuni au majina ya biashara waliopata leseni kupitia TNBP wanatakiwa kujisajili upya kwenye mfumo wa BOS kwa kutumia barua pepe na namba ya kitambulisho cha Taifa (Nida) kwa Watanzania au hati ya kusafiria kwa wageni. 

Aidha, mtu binafsi aliyekuwa na leseni kwenye mfumo wa TNBP, anapaswa kujisajili kupitia mfumo wa BOS kwa kutumia barua pepe aliyotumia katika mfumo wa TNBP ili kuweza kuona leseni za awali.

BRELA imefafanua kuwa kwa upande wa huduma nyingine kama usajili wa kampuni, hataza, alama za biashara na huduma pamoja na maombi yanayoendelea zitaendelea kutolewa kupitia mfumo wa Online Registration System (ORS).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: WABUNGE WAKIJADILI HOTUBA YA WIZARA YA NISHATI BUNGENI

🔴LIVE: WABUNGE WAKIJADILI HOTUBA YA WIZARA YA NISHATI BUNGENI

Nukta TV

Kupigwa risasi: Sababu vifo 197 katika matukio ya ghasia Oktoba 29

Kupigwa risasi: Sababu vifo 197 katika matukio ya ghasia Oktoba 29

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.