Nchi 10 zilizoongoza kwa uwekezaji (FDI) Tanzania 2024

April 25, 2026 4:08 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Uwekezaji wa kigeni nchini Tanzania ulikua kwa asilimia 12.1 katika hisa (stock) mwaka 2024, kwa mujibu wa Ripoti ya Uwekezaji Tanzania 2025, mwenendo unaobainisha imani ya wawezaji wa nje nchini. 

Katika mwaka huo, ripoti hiyo inabainisha kuwa uwekezaji wa kigeni pia ulikua kwa asilimia 17.1 kwa fedha zinazoingia nchini (inflows), hatua inasaidia kuingiza fedha za kigeni.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) hivi karibuni inabainisha kuwa kiasi cha uwekezaji (FPI) kilifikia Dola za Marekani bilioni 24.75 ambapo asilimia 87.7 ilitokana na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) na asilimia 11.2 kutoka uwekezaji mwingine (OI). 

Mafanikio haya yalichangiwa na kuongezeka kwa mtiririko wa FDI, hasa kupitia uwekezaji wa faida zilizorejeshwa (reinvestment of earnings) na mikopo ya muda mrefu kati ya makampuni yanayohusiana.

Kwa upande wa nchi zilizoongoza kuwekeza nchini Tanzania, Uingereza ilisalia kuwa mwekezaji mkuu kwa mwaka wa tatu mfululizo ikimiliki asilimia 26.9 ya hisa zote za uwekezaji.

Mwaka 2023, Uingereza iliwekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni 5.13 za Marekani baada ya kuwekeza Dola bilioni 3.95 mwaka 2022.

Kwa mwaka 2024, kuongezeka kwa uwekezaji kutoka Uingereza kunahusishwa na ununuzi wa hisa zilizokuwa zikimilikiwa na wawekezaji kutoka Canada na visiwa vya Cayman katika sekta ya madini. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Nukta TV

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Nukta TV

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni  iwe nzuri

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni iwe nzuri

Nukta TV