Sababu Mbowe kuonana na Rais Samia baada ya kutoka gerezani

March 8, 2022 2:45 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mbowe asema alipata wito kutoka Ikulu.
  • Asema alifanya hivyo kuendeleza falsafa ya maridhiano.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema angekuwa “mjinga” kukataa fursa ya kuona Rais Samia Suluhu Hassan muda mfupi baada ya kutoka gerezani kwa sababu aliitafuta kwa muda mrefu ili kuweka msingi wa maridhiano ya kitaifa kuhusu maendeleo ya Tanzania. 

Rais Samia alikutana na kufanya mazungumzo na Mbowe Machi 4, 2022 saa chache baada ya Mwendesha Mashtaka (DPP)  kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi namba 16 ya mwaka 2021.

Katika kesi hiyo, Mbowe na wenzake watatu Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohammed Ling’wenya walikuwa wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali ya ugaidi.

Mbowe aliyekuwa akizungumza mkoani Iringa leo wakati Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) likiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani amesema tangu mwaka jana Rais Samia alipoingia madarakani alitafuta fursa ya kuonana naye lakini hakupata.

Amesema alipata fursa hiyo muda mfupi baada ya kutoka gerezani ambapo alipokea wito kutoka Ikulu wa kuonana na Rais na hakusita kuitikia na angekataa angekuwa mjinga kwa sababu anaamini katika maridhiano.

“Kesi yetu ilipofutwa nilipokea ujumbe wa Mheshimiwa Rais Mama Samia kutaka tuonane haraka iwezekanavyo kwa sababu mbalimbali niliridhia,” amesema Mbowe na kubainisha kuwa mara ya mwisho kuonana rasmi na kiongozi mkuu wa nchi ilikuwa mwaka 2015 wakati wa uongozi wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Amesema kwa nafasi aliyonayo Rais ndiye mwenye funguo za vikwazo vingi vinavyosababisha simanzi ya muda mrefu kwa Taifa letu hasa zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambao amedai kuwa ulivurugwa.

“Kwa hiyo nilipopata mwaliko siku ile ile natoka gerezani nikathibitisha nitakwenda . Kamwe sikuruhusu uchungu na maumivu binafsi vinipe upofu na kiburi cha kutokuiona heshima niliyopewa na Rais,” amesisitiza Mbowe.  

Amemshukuru Rais kwa nafasi hiyo ya mapema ya kuonana naye na kufungua nafasi ya mashauriano na maridhiano kuhusu mstakabali wa Taifa na demokrasia.


Soma zaidi:


Aidha, amesema baada ya kutoka gerezani hana kinyongo na kisasi na mtu yeyote huku akihimiza Watanzania kuishi kwa upendo, amani, utulivu na kuvumiliana licha ya utofauti wa itikadi za kisiasa. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais Samia na Mbowe katika mazungumzo yao walijikita katika ujenzi wa nchi hasa kuzingatia misingi ya kufanya kazi kwa pamoja na maridhiano.

“Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki,” ilisema taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus.

Aidha, taarifa hiyo ilieleza kuwa Mbowe alimshukuru Rais Samia kwa kuonyesha kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga Taifa la Tanzania ni kusimama katika haki.

Mbowe alisema walikubaliana kufanya siasa za kistaarabu na za kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipaswavyo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
21 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV