Rais Samia: Suala la Wabunge 19 tuichie mahakama

March 8, 2023 1:11 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya Mbowe na Sharifa kumuomba atizame kwa jicho la tatu.
  • Asema pamoja na urais si rahisi kuingilia suala hilo.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuingilia kati suala la Wabunge 19 wanaodaiwa kuwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kutaka mahakama iachwe ifanye kazi yake.

Rais Samia aliyekuwa akihutubia kongamano la Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) leo Machi 8, 2023 mkoani Kilimanjaro ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maombi ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe la kutaka wabunge hao waondolewe Bungeni kwa sababu chama hicho hakikuwateua na tayari kilishawavua uanachama.

“Naomba niwaambie tuache mkondo ule uendelee, tutizame mbele yanayokuja, si rahisi mimi kama Rais kutia mkono huko,” amesema Rais Samia.

Kauli ya Rais Samia kuhusiana na jambo hilo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na maelfu ya wafuasi na wanachama wa Chadema ambao mara kadhaa walikuwa wakimkumbushia katikati ya hotuba yake ambapo baadhi walisikika wakisema “Covid-19”.


Soma zaidi


Kabla ya Mbowe kutoa ombi hilo, Mwenyekiti wa Bawacha Taifa Sharifa Suleiman naye alimuomba Rais kulitazama jambo hilo kwa jicho la tatu.

“Natambua kuwa si vema kuzungumzia kesi ambayo ipo mahakamani, lakini kwa niaba ya Bavicha nakuomba ulitizame hili kwa jicho la tatu, “ amesema Sharifa.

Itakumbukwa wabunge 19 wanaolalamikiwa akiwemo Halima Mdee na Esther Matiko, wanadaiwa kughushi nyaraka zilizowatambulisha kama wabunge wa viti maalumu kutoka Chadema ambapo chama hicho kilikana kuhusika na kuwavua uanachama Mei 11, 2022.

Julai 24, mwaka 2022 wabunge hao walifungua shauri mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama wakisema hawakuridhishwa na mchakato kwani walipokea vitisho na hawakupewa nafasi ya kusikilizwa.

Pamoja na jambo hilo kuzua mijadala mbalimbali Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Akson mara kadhaa amesikika akisema uhalali au ubatili wa wabunge hao kuwepo bungeni utabainika pale tu mahakama itakapotoa maamuzi yake.

Kesi hiyo ya Wabunge hao inatarajiwa kuendelea Machi 9 na 10 ambapo baadhi ya viongozi wa Chadema wataitwa kutoa ushahidi wao.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

🔴LIVE: HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA IKISOMWA BUNGENI

Nukta TV

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Fahamu kuhusu Virusi vya ‘Hantavirus’ na nini chanzo chake ?

Nukta TV