Unavyoweza kukabiliana na tatizo la uchovu uliopitiliza

May 18, 2021 9:16 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa kukaa mbali na pombe, dawa za kulevya pamoja na tumbaku.
  • Inashauriwa kuonana na daktari kwani uchovu ukiendelea, utapata changamoto za kihisia.

Dar es Salaam. Uchovu pia ni tatizo la kiafya ambalo mbali na uwezo wa kuambatana na magonjwa mengine kama homa na maumivu ya viungo, tatizo hilo linaweza kuathiri utendaji kazi wako wa kila siku na kukurudisha nyuma kimaendeleo.

Tatizo hilo ambalo kwa lugha ya kitaalamu huitwa “fatigue” ni hali ya kuhisi uchovu wa mwili na kukosa nguvu za kufanya shughuli mbalimbali.

Uchovu huo husababishwa na mambo mbalimbali lakini tovuti ya afya ya healthline.com imesema sababu kuu ni mtindo maisha, afya ya mwili na hali ya afya ya akili ya mtu.


Soma zaidi


Kwa upande wa mtindo wa maisha, mtu anaweza kupata changamoto ya uchovu ikiwa hapati muda mzuri wa kupumzika, kuwa na uzito uliopitiliza, huzuni, matumizi ya pombe mara kwa mara, matumizi ya madawa za kulevya na kushindwa kula mlo wenye virutubisho.

Afya ya mwili inaweza kusababisha uchovu pale unapokuwa na magonjwa au maambukizi. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kumpatia mtu uchovu ni pamoja na mafua, saratani, kisukari, magonjwa ya figo, sonona na magonjwa ya ini.

Kwa upande wa afya ya akili, uchovu unaweza kusababishwa na hali ya kuwa na wasiwasi au huzuni.

Unawezaje kukabiliana na changamoto hiyo? Tazama hii video fupi kujifunza zaidi.

Enable Notifications OK No thanks