Sababu za vioo vya magari kuwa na madoa meusi

TULINAGWE MALOPA 0255Hrs   Disemba 17, 2019 Safari
  • Alama za madoa hayo hutumika kushIkilia kioo kisipate hitilafu ya kuanguka au kuvunjika.
  • Alama hizo zimechukua nafasi ya vishikizio vya chuma vilivyokuwa vinatumika awali.
  • Bado madereva wengi hawajui matumizi ya alama hizo. 

Dar es Salaam. Kama ni mmiliki wa gari au ni msafiri mzuri kwa kutumia magari binafsi, bila shaka umewahi kuona mwonekano fulani katika vioo vinavyozunguka gari lako ambao ni  alama za vidoti vidogo vidogo vyeusi katika ukingo wa vioo hivyo.

Alama hizo siyo za bahati mbaya. Zimewekwa kwenye magari mengi yanayotumika kipindi hiki cha ukuaji wa teknolojia ya kisasa. Kazi kubwa ya alama hizo kusaidia kushikilia kioo wakati wa kushusha na kupandisha ili kisiharibike au kuvunjika. 

Alama hizo kwa kawaida zimetengenezwa kwa rangi iliyochanganywa na gundi inayotumika maalum katika magari binafsi.

Teknolojia hiyo ya alama za vioo imechukua nafasi ya zamani ya vishikizio vyenye asili ya chuma ambavyo vilikuwa vinatumika kushikilia kioo.

Licha ya kufanya kazi ya ya kusaidia kioo kushikika vizuri, lakini pia husaidia kupunguza joto kwenye vioo hivyo, jambo linalosaidia kupunguza hatari ya vioo kuvunjika mara kwa mara ikilinganishwa na vishikizio vya chuma ambavyo pia havina muonekano mzuri. 


Zinazohusiana:


Hata hivyo,  ni madereva wachache wanafahamu maana ya alama hizo zinapokuwa katika kioo cha gari na baadhi yao wamefikia hatua hata ya kuzitoa, jambo lililosababisha kuvunjika kwa vioo vya magari yao.

Mmoja wa madereva taxi katika kituo cha Plam Beach jijini Dar es Salaam Danford Elias anasema amewahi kujaribu kuondoa alama hizo na kioo hakikudumu muda mrefu kikaachia. 

“Kuna mambo mengi tunafanya kwa kutokujua. Mimi nilidhani ni urembo ila mimeshabadilisha kioo cha gari yangu kwa kutoa alama hizo bila kujua umuhimu wake,” amesema.

Related Post