Gari la kwanza la kimataifa linalotembea kwenye nyaya kuzinduliwa 2020

August 9, 2019 5:57 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Gari hilo litakuwa linasafirisha abiria kati ya China na Urusi.
  • Litakua linatumia dakika nane tu kusafiri kati ya mji wa Blagoveshchensk (Urusi)  na Heihe (China).
  • Litakua na uwezo wa kubeba abiria 60 kwa wakati mmoja. 

Gari la kwanza la kimataifa linatembea kwenye nyaya (cable car) ambalo litakuwa linasafirisha abiria kati ya China na Urusi kwa takriban dakika nane linatarajiwa kuzinduliwa mwaka ujao wa 2020.

Gari hilo litakuwa linafanya safari zake kati ya mji wa Blagoveshchensk (Urusi)  na Heihe (China) iliyopo mipakani mwa nchi hizo mbili. 

Mwanzilishi wa kampuni ya UNStudio, Ben van Berkel inayobuni na kutengeneza gari hilo wakati akihojiwa na mtandao wa Dezeen amesema wameanza mipango ya  kujenga miundombinu ya gari hilo la kwanza litakalounganisha nchi mbili na tamaduni zao. 

Gari hilo ambalo huvutwa kwa nyaya inayozungushwa kwa mota litakuwa linatembea katika njia kuu mbili za kimataifa kwenye nyaya nne, kila moja ikiwa na  uwezo wa kubeba abiria 60 na mizigo yao. 

Itachukua dakika saba na sekunde 30 kwa abiria kutoka China kwenda Urusi (au kinyume chake). Wakati halisi wa kusafiri kati ya nchi hizo mbili unatarajiwa kudumu kwa dakika tatu tu na sekunde 30.


Soma zaidi:


Abiria watakaohitaji kutumia usafiri huo watalazimika kukaguliwa na kupata vibali vya usalama vinavyohitajika kwa nchi hizo mbili. 

“Mfumo huu wa magari yanayotembea kwenye nyaya unatoa aina mpya ya usafiri wa umma ambao ni endelevu, wa haraka, wenye ufanisi na unaopatikana wakati wote,” amesema van Berkel katika taarifa yake. 

Magari yanayotembea kwenye nyaya, pia yanatumika kama kichocheo cha utalii kwa sababu yanawawezesha abiria kuona manthari ya miji na fahari yake wakiwa angani. 

Ujenzi wa mfumo huo wa magari yanayotembea kwenye nyaya na vituo vya abiri katika miji yote miwili unatarajia kuanza mwaka ujao kabla ya uzinduzi rasmi. Muonekano wa mfano wa miundombinu ya gari linalotembea juu ya nyaya itakavyokuwa baada ya kujengwa  kati ya mji wa Blagoveshchensk (Urusi)  na Heihe (China) iliyopo mipakani mwa nchi hizo mbili. Picha|Mtandao.

Enable Notifications OK No thanks