Rais Samia kuhudhuria baraza la kuu la Umoja wa Mataifa

September 4, 2021 7:12 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mkutano wa baraza hilo utafanyika kati ya Septemba 21 hadi 27, 2021.
  • Rais Samia atahudhuria kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe Machi mwaka huu.

Dar es Salaam. Rais wa Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria  mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN Council) utakaochofanyika mwezi huu, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ateuliwe  kuwa Rais wa Tanzania mwezi Machi 2021.

Mkutano huo wa 76 unatarajiwa kufanyika kati ya Septemba 21 hadi 27, 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema kwa sasa wanasubira maamuzi ya Serikali ya Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iwapo nchi wanachama watashiriki kwa njia ya mtandao au watasafiri kwenda nchini Marekani.

“Taadhima yetu ni kushiriki, iwe ana kwa ana au mtandao, Muheshimiwa rais ameshasema atashiriki. Na unajua hii ndiyo mara yake ya kwanza anashiriki kama Rais wa nchi atakuja,” amesema Mulamula wakati akihojiwa na  idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Tanzania ilikuwa haiwakilishwi na kiongozi mkuu wa nchi badala yake ulikuwa unatumwa ujumbe maalum kufikisha ajenda katika baraza hilo.

Hatua ya Rais Samia kukubali kuhudhuria mkutano huo, huenda ni jitihada za Serikali kufufua na kuimarisha uhusiano na diplomasia ya kimataifa zikiwemo nchi rafiki ili kufaidika katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka ni mkutano muhimu unaowakutanisha wakuu wa nchi wanachama wa baraza hilo na wataalam mbalimbali duniani kujadili ajenda za maendeleo ikiwemo utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s).

Pia hutolewa fursa kwa nchi kutoa ajenda na misimamo yao kuhusu masuala mbalimbali yanayojadiliwa baraza hilo. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV