Rais Samia: Baraza la Amani na Usalama la AU limetusaida kukabiliana na ugaidi Afrika

May 25, 2024 11:40 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Baraza hilo limejipatia mafanikio mengi katika kuimarisha ulinzi na usalama Afrika.
  • Changamoto zinazolikabili baraza hilo ni pamoja na vita na nchi wanachama kuingiliwa kimaamuzi na mataifa ya nje.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu hassan amesema Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika(AU) limezisaidia nchi za Afrika kujilinda dhidi ya matishio ya kiusalama ikiwemo ugaidi.

Baraza la Amani na Usalama ni chombo cha juu cha maamuzi kuhusu masuala ya amani na usalama kwenye Umoja wa Afrika likiwa na jukumu la kuzuia kutokea kwa migogoro, kusuluhisha au kukabiliana nayo pale inapojitokeza.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya baraza hilo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 25, 2024 amesema mbali na kujlinda dhidi ya ugaidi baraza hilo lililooanzishwa mwaka 2004 limezisaidia nchi za Afrika hususani zilizokabiliwa na vita kujiimarisha. 

“Tangu kuanzishwa kwake baraza limepata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzishwa majadiliano ya upatanishi hadi kusaidia nchi kujengwa upya baada ya vita (Post war),” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia aliwaambia wahudhuriaji kuwa baraza hilo hilo limejidhatiti katika kusimamia misingi ya haki za binadamu, demokrasia na utawala bora, pamoja na kuangazia ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika masuala ya amani na usalama.


Soma zaidi:Mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani yapaa kwa asilimia 7


Maadhimisho hayo yanafanyika nchini Tanzania ikiwa bado kuna nchi barani Afrika zinakabiliwa na na machafuko ya kisiasa yanayopelekea watu kupoteza maisha  ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Somalia na nyinginezo ambapo Rais Samia ameitaja hali hiyo kama changamoto inayolikumba baraza hilo.

“Tumeshuhudia migogoro ya uhalifu wa kimataifa na ukosefu wa hatua madhubuti za kuizuia, kwa ujumla bado hatujanyamazisha kabisa bunduki barani Afrika, changamoto nyingine kubwa ni mabadiliko ya kikatiba ya Serikali na urejeshaji wa utaratibu wa kikatiba,”  amebainisha Rais Samia.

Baadhi ya wahudhuriaji wa maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika(AU) katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.Picha|Ikulu.

Awali Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU ) Moussa Faki Mahamat alifafanua changamoto ya kikatiba kuwa miongoni mwa sababu zinazofanya baadhi ya chaguzi Afrika kukosa uangalizi kutoka baraza hilo kutokana na nchi wanachama kushindwa kutoa ratiba ya tarehe za uchaguzi kwa wakati.

Pia amesema changamoto nyingine ni nchi za Afrika kuingiliwa kimaamuzi na mataifa ya nje, hatua inayosababishwa na kukosekana kwa umoja na ushikamano baina ya nchi wanachama.

Pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo Rais Samia amewataka wahudhuriaji wa maadhimisho hayo kujikita katika kutafuta suluhu ya changamoto hizo na kuzitatua.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV