Rais Samia atengua uteuzi wa Diwani Athumani

January 5, 2023 1:01 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Amteua Mululi Majula Mahendeka kuchukua nafasi yake ya kusimamia shughuli za ofisi hiyo nyeti nchini Tanzania. 
  • Atengua uteuzi wake baada ya kumteua Januari 3, 2022.

Dar es Salaam. Siku ya leo huenda inaweza isiwe nzuri kwa Kamishna Diwani Athumani Msuya baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumfuta kazi ya Katibu Mkuu Ikulu huku akimteua Mululi Majula Mahendeka kuchukua nafasi yake ya kusimamia shughuli za ofisi hiyo nyeti nchini Tanzania. 

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa leo mchana Januari 5, 2023 inaeleza kuwa Mahendeka alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.

Kutenguliwa kwa Diwani kunahitimisha safari ya saa chache za kukaa katika nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na Rais Samia kuwa Katibu Mkuu Ikulu Januari 3, 2022.  

Kabla ya Diwani kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), nafasi aliyodumu nayo tangu alipoteuliwa na Rais wa wakati huo, Hayati John Magufuli Septemba 12 mwaka 2019.

Alishikilia nafasi hiyo kutoka kwa Dk Modestus Kipilimba ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Namibia.

Kabla ya Diwani kushika wadhifa huo wa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa alikuwa mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

 

Ni panga pangua

 Rais Samia akizungumza Januari 3, 2023 wakati akitangaza mabadiliko hayo aliyosema ataendelea kuyafanya ambayo pia yalimhusu  aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga aliyeteuliwa kwenda Marekani kuwa Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa (UN).

Kattanga anakwenda kuchukua nafasi ya Profesa Kennedy Gaston ambaye amerudishwa nchini. 

 

Balozi Kattanga ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi Machi 31, 2021 alichukua nafasi ya Dk Bashiru Ali ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kuteuliwa.

Kabla ya nafsi hiyo ya ukatibu mkuu kiongozi, Kattanga alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV