Kamishna Diwani Athumani bosi mpya Usalama wa Taifa

September 12, 2019 10:59 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Kabla ya uteuzi, Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), nafasi aliyoitumikia tangu Septemba 6, 2018. Picha|Michuzi.


  • Rais John Magufuli leo amemteua na kumuapisha Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). 
  • Kamishna Diwani amechukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine.
  • Kabla ya uteuzi, Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo amemteua na kumuapisha Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). 

Kamishna Diwani amechukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine. 

Kabla ya uteuzi, Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), nafasi aliyoitumikia tangu Septemba 6, 2018. 

Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka Kamishna Diwani kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kuweka mbele maslahi ya Taifa. 

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Diwani Athumani alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Pia amewahi kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera na Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Shinyanga na Mbeya. 

Dk Kipilimba ni nani?

Dk Kipilimba aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Agosti 24, 2016 akitokea Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambako alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu.

Pia amewahi kuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambako alifanya kazi kuanzia mwaka 2011.

Kabla ya kufanya kazi hiyo, Dk Kapilimba alikuwa Meneja wa Udhibiti Mfumo wa Majanga wa BoT, nafasi aliyoshikilia kutoka mwaka 2009 hadi 2011 alipopandishwa cheo kuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga Benki Kuu ya Tanzania.

Dk Kipilimba amebobea katika sayansi ya kompyuta ambapo elimu yake aliipata kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Canterbury na Chuo Kikuu Cha Salford vya nchini Uingereza. 

Enable Notifications OK No thanks