Rais Samia atengua uteuzi Mkuu wa Wilaya Mbarali, wakurugenzi wanne

January 24, 2023 2:51 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni utenguzi wa pili tangu mwaka 2023 uanze.
  • Utenguzi huo ulianza tangu Januari 22.

Dar es salaam. Huenda leo itakuwa siku mbaya kwa wakurugenzi watendaji wanne wa halmashauri na mkuu wa wilaya mmoja baada ya teuzi zao kutenguliwa. 

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi wa viongozi watano ngazi ya wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na Kusainiwa na Mkurugenzi wake Zuhura Yunus leo Januari 24, 2023, utenguzi huo ulianza Januari 22 mwaka huu.

Viongozi wengine waliotenguliwa ni Msongela Nitu Palela aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Michael Augustino Matomora aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Wengine ni Linno Pius Mwageni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga pamoja na Sunday Deogratius Ndori aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

Huu si utenguzi wa kwanza kwa Rais Samia tangu mwaka 2023 uanze. Itakumbukwa kuwa Januari 5 mwaka huu, Samia alitengua uteuzi wa Diwani Athumani kuwa Katibu wa Ikulu na kumpa nafasi hiyo Mululi Mahendeka.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

Nukta TV

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

Nukta TV