Rais Samia ashiriki sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Nigeria

May 29, 2023 1:21 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni Rais wa awamu ya 16 kuongoza taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.
  • Atangaza vipaumbele vitano vya Serikali, atangaza vita dhidi ya ugaidi, na kuimarisha usawa.

Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu Hassan ameungana na viongozi mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Nigeria, Bola Tinubu, aliyeapishwa leo Mei 29, 2023 kufuatia kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Februali 25, 2023.

Sherehe hizo zimefanyika  katika viwanja  vya ‘The Eagle Square’ nchini Nigeria ambapo viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune, Katibu mkuu wa Baraza la Mawaziri nchini Kenya  Musalia Mudavadi, ambaye amemuwakilisha Rais wa nchi hiyo William Ruto pamoja na wajumbe kutoka nchi za Marekani , Uingereza na China ni baadhi ya viongozi wengine waliofika katika sherehe hiyo.

Rais Bola Tinubu  aliyeapishwa leo mbele ya umati wa wananchi wa Nigeria anakuwa Rais wa 16 kushika madaraka hayo tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1960.

Tinubu mwenye umri wa miaka 71 alishinda kiti hicho kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 Februari 2023 ambapo kwa mujibu wa tovuti ya ‘Premium Times’ ya nchini Nigeria Rais huyo alipata kura milioni 8.7 na kuwashinda wagombea wengine 17.

Sherehe hizo pia zilihusiha kuapishwa kwa Makamu wa Rais mteule Kashim Shetima aliyeapa mbele ya jaji mkuu wa nchi hiyo Olukayode Ariwoola.


Soma zaidi


Mahusiano ya Tanzania na Nigeria

Ushiriki wa Rais Samia katika sherehe hizo ni mwendelezo wa mahusiano baina ya mataifa haya mawili ambayo yamekuwa yakishirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara yaliyoimarika zaidi mwaka 2022.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje Liberata Mulamula biashara kati ya nchi hizo imeongezeka kutoka Sh23 bilioni mwaka 2020 hadi Sh24 bilioni mwaka 2021.

Kama matunda ya ushirikiano huo ulioasisiwa mwaka 1962, Tanzania inanufaika na uwekezaji uliofanywa na  raia wa Nigeria nchini akiwemo Aliko Dangote ambaye anazalisha saruji kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Rais mteule wa Nigeria Bora Tinubu (wa pili kulia) akila kiapo cha urais mbele ya jaji mkuu wa Nigeria Olukayode Ariwoola (wapili kushoto).Picha|Ikulu/Twitter.

Tinubu aweka wazi kanuni zitakazoongoza Serikali yake

Mara baada ya kuapishwa Rais Tinubu amehutubia wahudhuriaji wa sherehe hizo na kuweka wazi kanuni tano zitakazoongoza Serikali yake inayoingia madarakani.

“Kanuni zitakazoongoza utawala wetu  ni rahisi Nigeria itaongozwa bila upendeleo kwa mujibu wa katiba na utawala wa sheria,”amesema Rais Tinubu.

Rais huyo ameongeza kuwa Serikali yake italilinda taifa dhidi ya ugaidi na aina zote za uhalifu unaotishia amani na utulivu,kurebisha uchumi, pamoja na kuhakikisha usawa kwa wanawake na vijana. 

“Serikali yetu itaendelea kuchukua hatua madhubuti kama vile kutetea utamaduni wa utoaji mikopo, kupinga rushwa na kuimarisha ufanisi wa vyombo mbalimbali vya kupambana na rushwa,”amesema.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV