Rais Samia amlilia Lawrence Mafuru

November 9, 2024 1:59 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kufariki Novemba 9, 2024 akipatiwa matibabu nchini India.

Arusha.  Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Nyasebwa Mafuru aliyefariki leo Novemba 9, 2024.

Taarifa ya Ikulu Mawasiliano inabanisha kuwa  Mafuru amefariki leo Novemba 9, 2024 katika Hospitali ya Apollo nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kupitia taarifa yake iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijami Rais Samia ametoa pole kwa watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu, jamaa na marafiki.

“Ninatoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu…

…Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali,” amesema Rais Samia katika mitandao yake ya kijamiai ikiwemo Instagram.

Enzi za uhai wake Mafuru alitumikia nafasi mbalimbali katika Serikali za awamu tofauti ikiwemo ya Rais Samia kama Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa nafasi aliyoitumikia tangu Julai 5, 2023 tume hiyo ilipoundwa.

Kabla ya kuitumikia nafasi hiyo Mafuru alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi). 

Pia aliwahi Mkurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Msajili wa Hazina na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  katika Serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV